FURSA ZILIZOPO KATIKA WILAYA YA LONGIDO
Wilaya ya Longido ni moja kati ya Wilaya zenye fursa za uwekezaji
Fursa
hizo ni pamoja
na:
-
•
Wilaya ipo mpakani na ni lango la mazao ya kilimo na mifugo yanayokwenda nchi
jirani hivyo ina nafasi ya kuwekeza katika masoko ya ndani na kimataifa ya
mazao ya mifugo na kilimo.
•
Wilaya inao umeme wa uhakika kutoka gridi ya Taifa .
•
Wilaya inayo maeneo mengi yenye maji ya mtiririko na chini ya ardhi katika
maeneo yanayopendekezwa k
wa uwekezaji na pia
uko mradi mkubwa wa maji
mririko toka Mto
Simba Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro
,
Mradi huu
utaiwezesha mji wa Longido kuwa na maji
•
Wilaya ina viwanja vya ndege vidogo 3 Muryatata, Mundarara, Gelai Meirugoi na
inayo maeneo mengi
yanayofaa kwa kujenga viwanja vipya vya ndege
(Wosiwosi, Oltepesi, Sinya, Mundarara, na Meirugoi.
•
Kuwepo kwa ardhi ya kutosha kwa uwekezaji wa aina mbalimbali ikiwemo
malisho, ujenzi wa hospitali ya wilaya (88,825.59m
2
) ujenzi wa chuo cha ufundi
ekari 39,
ujenzi wa “Campsite”, uvunaji madini na umeme wa uhakika kutoka
gridi ya Taifa.
•
Wilaya ina maeneo yenye vivutio pekee vya utalii kama chemichemi za maji ya
moto, makazi ya kiasili ya kimaasai, mlima wa nyani (Magadini), mlima wenye
volcano hai (Oldonyo Le
ngai) na mlima Longido.
•
Uwepo wa maeneo ya vitalu vya uwindaj
i. Hivi sasa wilaya ina vitalu 6
vya
uwindaji na kuna maeneo mengi ya kujenga hoteli za kitalii.
3
•
Kuwepo kwa ndege aina ya Flamingo na magadi soda eneo la ziwa Natron vijiji
vya Wosiwosi, Magadi
ni na Gelai Meirugoi.
•
Wilaya ina maeneo yenye madini yakiwamo ruby, dhahabu, chokaa (limestone)
na mengine.
•
Wilaya inayo barabara ya lami inayounganisha mkoa wa Arusha na nchi jirani ya
Kenya (Km. 104) ambayo ni kiungo kikuu cha mawasiliano.
•
Wilaya inazo
barabara nyingi zinazopitika muda wote (Km. 458) na hivyo
kurahisisha usafiri na usafirishaji Endelea
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM