Na Saumu Kweka
Kikao cha Madiwani kilicho fanyika mapema leo tar 17 August katika ukumbi wa Mwl.J K Nyerere cha kupitia hoja za matumizi ya fedha za halmashauri.
Kikao hicho kilicho endeshwa na Mwenyekiti Mh,Sabore Mollaimet na Makamu Mwenyekiti Esupati Ngulupa na na kuhudhuriwa na wageni kutoka Mkoani,katika kujadili nyaraka za hoja za matumizi ya fedha
Aidha Mwenyekiti Mh Sabore aliwaomba watoa taarifa za hoja na waandaaji kuwa makini wanapo toa taarifa hizo ili kuhakikisha hoja zao zina kuwa sahihi na zenye ukweli.
Hatahivyo Wageni walio hudhuria kikao hicho kutoka Mkoani waliwataka watoahoja na Halmashauri kwa ujumla kushirikiana vyema na Idara ya Ukaguzi ili kuweza kutoa taarifa zenye usawa.
Pia Wageni hao waliongezea kwakuwaomba kuwa makini na Matumizi ya fedha, Manunuzi,Uwasilishaji mikataba ya Zabuni,na Mikataba ya vibarua /watumishi wanao ajiriwa isainiwe ilikuepuka hoja zisizo na ulazima,Hatua za kinidhamu zichukuliwe na kuwa makini kwenye utunzaji wa kumbukumbu za Halmashauri.
Aidha Makamu Mwenyekiti Mh,Esupati alimaliza kwa kuwataka Waandaaji wa taarifa za hoja kuongeza umakini ili kuepuka hati zenye makosa kupitia makosa madogo madogo yaliyo jitokeza na kutokupata hati zenye mashaka katika Halmashauri.
Approved by Joseph Peter Mkumbwa
AgDICTO
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM