Na Johnson Ismail
Approved By Joseph Peter Mkumbwa. ICTO
Ufunguzi wa Mafunzo hayo ya Mfumo wakuandaa Bajeti wa PLANRES na FFARS yamefunguliwa rasmi leo kwenye ukumbi wa Mwal J.K Nyerere mafunzo hayo yatakayo chukua siku tano yakiwa na malengo yakuongeza ujuzi/maarifa juu ya mfumo mzima wa takwimu.
Mafunzo hayo yamejumuisha wakuu wa Idara na Vitengo,Maafisa Bajeti kutoka kwenye Idara na Vitengo pia Wajumbe wa CHMT ambao kwapamoja watajihusisha na utaratibu mzima wa uandaaji wa bajeti kwenye maeneo yao kulingana na shughuli zitakazo fanyika na mfumo mzima wa matumizi kulingana na bajeti zao.
Hatahivyo mafunzo hayo yamefunguliwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye ni Afisa utumishi (W)Longido Ndg.Steven Mbombe kwa kuwataka watumishi hao kuzingatia mafunzo hayo kwakuwa mpango wa Bajeti ndio dira ya shughuli zitakazo tekelezwa kwa mwaka Mzima.
“Bajeti ni mpango hivyo kushindwa kupanga malengo itapelekea kushindwa kutekeleza malengo,hivyo kila mmoja kwa nafasi yake awe makini kujifunza na kuyaelewa mafunzo hayo”.amesemsa Kaimu Mkurugenzi.
Hatahivyo Afisa Mipango wa Halimashauri ya Longido Peter Ngusa amesema kuwa Mafunzo haya yana lenga kuwa jengea uwezo Watumishi juu ya mfumo wa PLANRES na FFARS ambao umeboreshwa na mifumo mingine kama Epicor,LGRCIS na mifumo mingine.
Aidha Afisa Mipango Ngusa amesema kuwa mfumo huu umepunguza gharama kwa kuwa maandalizi yatafanyika kwenye mfumo yaani Online kadhalika na uwakilishaji wake ni tofauti na zamani ilikuwa lazima watu kusafiri kwenda kuwasilisha bajeti, hali ambayo kwa sasa haitakuwepo .
Pia washiriki wa Mafunzo hayo wakuu wa Idara,Vitengo Maafisa Bajeti,wali furahishwa na ufunguzi huo na kusema ni njia nzuri ya kuwafundisha kwani watakua wana tumia mafunzo hayo vizuri katika utendaji wao wa kazi na kuacha kutumia pesa nyingi kwaajili ya kusafiri kuwasilisha Bajeti.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM