Wajumbe wa Baraza la madiwani wa halmashauri ya Longido wamefanya mkutano wa kuwasilisha taarifa za kata za robo ya pili za kuanzia mwezi oktoba mpaka disemba 2017, Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Mkutano huo umehudhuriwa na madiwani wa kata 16 kati ya 18 katika wilaya ya Longido, Wakuu wa idara na vitengo na wadau mbalimbali kutoka halmashauri ya wilaya ya Longido
Madiwani hao waliweza kuwasilisha taarifa hizo wakiwa wameeleza mafanikio na changamoto wanazokumbana nazo katika nyanja za elimu, kilimo, ufugaji, utekelezaji wa miradi ya maendeleo , utunzaji wa mazingira ,kiuchumi na afya.
Hata hivyo baadhi ya changamoto zilizo bainishwa ni pamoja na utoro, upungufu wa madarasa ,nyumba za watumishi, mabweni, maabara, uhaba wa malisho, usafiri , maji safi na salama, madawati,vitendea kazi kwenye ofisi za umma.
Vilevile Katibu Tawala wa wilaya ya Longido ndg. Toba Nguvila alipata nafasi ya kuongea machache na amesisitiza baadhi ya mambo muhimu kama ugawaji wa fedha za TASAF kwa wasio na sifa, zoezi la kuweka ng'ombe chapa isimamiwe kwa makini, agizo la rais john pombe magufuli la kupiga marufuku kutoza mchango wowote kwa wanafunzi kwa ajili ya elimu, uhakiki wa watoto kwenda shule na madiwani kushiriki kwenye vikao husika.
Hivyo basi mkutano huo uliweka mikakati ya kutekeleza mipango ili kutimiza malengo.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM