Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Longido Ndg Jumaa Mhina anawatangazia wananchi wote wa Jimbo la Longido na wenye sifa ya kupiga Kura kujitokeza kwa wingi kesho siku ya Jumamosi tarehe 13.01. 2018 kwenda kupiga kura ya kumchagua Mbunge wa jimbo lao
Vituo vya kupigia kura vitafungulia kuanzia saa 01:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni hivyo wapiga kura wanatakiwa kutumia muda huo uliopangwa.
Uchaguzi utafanyika katika vituo vya kupigia kura vilivyotumika katika Uchaguzi mkuu was Raisi, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015.
Aidha anawataka wananchi hao kupiga kura kwa amani na utulivu na baada ya kupiga kura kuondoka kwenye kituo na kuendelea na shughuli nyingine.
Siku ya hiyo ya Uchaguzi in lazima mpiga kura afike kituoni na kadi yake ya mpiga kura na kama amepoteza kadi hiyo ataruhusiwa kupiga kura akiwa na leseni ya udereva,au hati ya kusafiria au kitambulisho cha uraia kilichotolewa na mamlaka ya vitambulisho vya Taiga (NIDA) kwa sharti LA majina yake kuwa katika mtiririko sawa na kwenye daftari LA wapiga kura na picha yake kufanana.
Pia hairuhusiwi kubaki kwenye kituo cha kupigia kura mara baada ya kupiga kura, kukaa kwenye mikusanyiko ya vikundi vikundi, kuvaa nguo inayoashiria rangi ya Chama chochote wala kufanya kampeni ya kushawishi mtu kumchagua mgombea fulani.
Msimamizi wa Uchaguzi amewahakikishia wananchi wote wa Longido kuwa hali ya Ulinzi na Usalama imeandaliwa vizuri kuhakikisha zoezi hilo linafanyika na kukamilika kwa amani na utulivu.
Wana Longido tumia haki yako ya kuchagua Mbunge kwa maendeleo ya Longido.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM