Ufugaji wa ng’ombe wa asili (zebu) kwa ajili ya nyama na maziwa.
Ufugaji wa ng’ombe wa kisasa (friesian, ayrshire, jersey) katika maeneo machache kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa.
Biashara ya kuuza ng’ombe sokoni (mfano, soko la Kimokouwa na Namanga).
Ufugaji wa mbuzi wa kienyeji kwa ajili ya nyama na maziwa.
Ufugaji wa mbuzi wa maziwa (mbuzi saanen na toggenburg) unaanza kuenea taratibu.
Mauzo ya mbuzi katika masoko ya ndani na nchi jirani (hasa Kenya).
Kondoo wa asili (red maasai na black head) wanaofugwa kwa ajili ya nyama na ngozi.
Wanafugwa kwa wingi kutokana na kustahimili mazingira ya ukame.
Kuku wa kienyeji wanaofugwa kwa chakula na kipato cha haraka.
Kuku wa kisasa (broiler na layers) wanaofugwa kwa biashara ndogo ndogo mjini Longido na Namanga.
Ufugaji wa nyuki (asali) unafanyika katika vijiji vya misitu na hifadhi kama Elerai, Ketumbeine na Engikaret.
Asali huuza ndani na nje ya wilaya.
Punda hutumika kama usafiri wa mizigo na pia huuzwa.
Ngamia wanaanza kufugwa hasa maeneo ya ukame kwa ajili ya maziwa na usafiri.
Bidhaa za mifugo kama maziwa, nyama, ngozi na asali zinauzwa ndani ya Longido na maeneo ya mipaka (Namanga).
Wafugaji wanashiriki kwenye minada ya kila wiki kuuza mifugo
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.