Jinsi ya Kupata Salary Slip Kupitia Mfumo wa TEHAMA: Watumishi Portal na ESS
Watumishi wa umma wanaweza sasa kupata salary slip zao kwa njia rahisi na ya kidijitali kupitia mifumo rasmi ya serikali: Watumishi Portal na ESS (Employee Self Service). Mifumo hii inalenga kuongeza uwazi na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa watumishi bila gharama yoyote.
Ili kupata salary slip kupitia Watumishi Portal, fuata hatua hizi:
Tembelea tovuti ya Watumishi Portal kupitia link iliyopo kwenye sehemu ya Tovuti Muhimu.
Jisajili kwa kuweka taarifa zako binafsi, ikiwemo:
Barua pepe (email address) – Ikiwa huna, unaweza kusaidiwa kufunguliwa bila gharama kwenye ofisi ya TEHAMA au UTUMISHI.
Cheki namba – Hii hupatikana kwenye salary slip zako za zamani au kutoka kwa Afisa Utumishi.
Baada ya kujisajili, ingia kwenye akaunti yako na pakua salary slip yako kila mwezi.
Unaweza pia kupata salary slip kupitia Mfumo wa ESS, ambao unatumika na baadhi ya Mamlaka au Taasisi:
Tembelea tovuti ya ESS ya taasisi yako.
Ingia kwa kutumia namba yako ya utumishi au cheki namba, pamoja na nenosiri lako.
Ndani ya mfumo, utaona kipengele cha Salary Slip ambapo unaweza kupakua slip za mishahara zako.
Ikiwa unapata changamoto katika usajili au matumizi ya mifumo hii, tafadhali fika katika ofisi ya TEHAMA au UTUMISHI ya Halmashauri yako kwa msaada wa moja kwa moja. Huduma hii hutolewa bila malipo yoyote
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.