"KUSOMA KWA BIDII, KUJIAMINI KUJITAMBUA NDIO SILAHA KUBWA YA MAFANIKIO KWA MTOTO WA KIKE."Ni maneno yake Afisa maendeleo ya Jamii Wilaya Ndugu Grace Mghase alipofika kutembelea na kuzungumza na watoto wa kike katika shule ya Sekondari ya Lekule kata ya Gelai Lumbwa Wilayani Longido.
Katika kusherehekea siku ya wanawake Dunia Ndugu Grace Mghase amewaasa watoto hao wakike Kuweka bidii kwenye masomo yao ili kufikia malengo yao ya maisha ya sasa na badae. Sambamba na hilo amewataka watoto hao kuacha tabia ya usiri na kuwa wazi kueleza changamoto zinazojitokeza na kuwakwamisha kutokufika ndoto zao kwa urahisi, "Watoto wazuri tumieni vema sanduku la maoni kueleza changamoto zenu zote zinazowakibili, maoni hayo yatasomwa na kufanyiwa Kazi Kwa haraka sana "Alisema Ndugu Grace.
Vile vile Afisa maendeleo ya jamii huyo pamoja na maafisa wengine wanawake waliofika shuleni hapo wametoa zawadi mbali mbali ikiwepo taulo za kike kwa wanafunzi hao ili ziwasaidie kujistiri, Sambamba na kuwafundisha matumizi bora na sahihi ya kutumia taulo hizo za kike pamoja na usafi.
Akishukuru kwa niaba ya wanafunzi wengine wa shule hiyo ya wasichana Lekule Mwanafunzi Anna Lukas wa kidato cha tatu amewashukuru sana wageni hao kwa kuona Kuna sababu ya Kuja kutembelea na kuzungumza na watoto wa kike, mwanafunzi huyo ameongeza kwa kusema kwamba elimu iliyotolewa ni nzuri na ina tija kwa Afya na ustawi wa maendeleo yao hivyo kuahidi kufanyia Kazi na kutopuuza yale yote walaofundishwa kwa faida ya maisha yao ya sasa na badae.
LONGIDO TUNATEKELEZA KWA VITENDO#
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAZI IENDELEE
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM