Wajumbe wa Baraza la madiwani wa halmashauri ya Longido wamefanya mkutano wa kuwasilisha taarifa za kata za robo ya nne za kuanzia mwezi Aprili mpaka Julai 2019, Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo ( Ukumbi wa Nyerere).
Mkutano huo umehudhuriwa na madiwani,Wakuu wa idara na vitengo na wadau mbalimbali kutoka halmashauri ya wilaya ya Longido.
Taarifa hizo ziliwazilishwa katika nyanja mbalimbali za elimu, maji,afya,kilimo,mifugo na uvuvi maendeleo ya jamii na miundombinu.
Pia madiwani hao waliweza kuwasilisha taarifa hizo wakiwa wameeleza mafanikio na changamoto wanazokumbana nazo katika nyanja za elimu, kilimo, ufugaji, utekelezaji wa miradi ya maendeleo , utunzaji wa mazingira ,kiuchumi, afya pamoja na miundombinu inayozidi kuharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha hasa katika kata ya Namanga.
Hata hivyo baadhi ya changamoto zilizo bainishwa ni pamoja na utoro wanafunzi mimba, upungufu wa madarasa ,nyumba za watumishi, mabweni, maabara, uhaba wa malisho, usafiri ,miundo mbinu za barabara, maji safi na salama, madawati,vitendea kazi kwenye ofisi za umma.
Vilevile mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ambaye ni afisa Ndug. Toba Nguvila kwa niaba ya mkuu wilaya amesema tayari serikali imekwisha tenga bajeti ya Billion 1.5 kwaajili ya ujenzi wa Chuo cha veta, na pia wako katika mchakato wa kupata maeneo ya ujenzi wa Gereza ndani ya wilaya ya Longido Miradi ambayo itasaidia kusogeza huduma za kimaendeleo kama Maji, umeme, miundombinu mizuri n.k, lakini pia kusogeza huduma karibu za mafunzo ya Veta.
Mwenyekiti wa kikao Mhe. Sabore Molloimet wakati anafunga mkutano wa baraza alisema anaomba halmashauri kufanyia kazi changamoto zilizowasilishwa na waheshimiwa madiwani wakati wanawasilisha taarifa zao na kuwasihi watumishi wote kuendelea kuziunga mkono jitihada za serikali ili washirikiane kuibadilisha Longido kwa maendeleo.
Aidha Mhe. Molloimet amewasii wajumbe kuwajibika ikiwa pamoja na kutoa taarifa kwa wananchi wao maana taratibu hizo zipo kisheria na kuwataka kusimamia kwa makini fedha zinazotolewa na serikali kwa kuzielekeza sehemu husika na kuhakikisha haipotei hata senti jambo ambalo litajenga uhaminifu kwa serikali na wananchi.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM