Wilaya ya Longido imepatiwa kiasi cha tani 40 za mbolea ya kupandia, tani 40 za mbolea ya kukuzi na tani 8 za mbegu za mahindi kwa ajili ya wakulima 800 katika mfumo wa pembejeo zenye ruzuku ya serikali katika msimu wa kilimo wa 2016/2017. Aidha, kikao cha Kamati ya Pembejeo ya Wilaya kilichoketi tarehe 16/01/ 2017 kilipitisha mgawo na kupanga bei elekezi za kuuza pembejeo hizo katika vituo ambavyo ni makao makuu ya kila Kata ambazo zitapatiwa pembejeo. Sambamba na hilo nawatambulisha kwako Mawakala Wiana Agrovet na Atau Agrovet ambao watahusika za usambazaji wa pembejeo katika Wilaya ya Longido kwa msimu wa kilimo wa 2016/2017. Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe Daniel Chongolo leo alikuwa mgeni rasmi katika Kikao Maalum cha kuvunja Bodi ya Afya ya Wilaya ya Longido ambayo imemaliza muda wake kwa mujibu wa Sheria baada ya kuhudumu kwa mika mitatu. Bodi hiyo iliyokuwa chini ya Uenyekiti wa Ndg Isack Ndekero iliundwa tarehe 18/04/2013 ikiwa na Wajumbe 11.
Mhe Chongolo akivunja Bodi hiyo aliipongeza kwa kuwa mstari wa mbele kupigania upatikanaji wa Huduma bora za Afya ndani ya Wilaya licha ya changamoto nyingi zilizopo ikiwemo changamoto za kimazingira, ukosefu wa vitendea kazi, upungufu wa watumishi wa Sekta ya Afya na ukosefu wa fedha kutosheleza mahitaji mbalimbali katika Sekta hiyo. Pamoja na hayo Bodi hiyo inajivunia mafanikio kadhaa ikiwemo kufanikiwa kuhamasisha Jamii kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) ambapo wanachama waliongezeka kutoka 16% na kufikia 34% sawa ma Wanachama 8,412. Bodi pia ilihimiza Ujenzi wa Jengo la X-Ray katika Kituo cha Afya cha Longido ambao unaendelea, kupatikana kwa Huduma za Upasuaji katika Kituo cha Afya Longido na Enduimet, kuwa na mgawanyo mzuri wa Watumishi wa Sekta ya Afya katika Vituo vya Huduma, na Vituo vyote 26 vya kutoa Huduma za Afya kufungua Akaunti za Benki. Aidha Bodi iliweza kuhamasisha Wanawake kujifungulia kwenye Vituo vya Afya badala ya Wakunga wa Jadi, ufuatiliaji wa upatikanaji wa Madawa, na kufuatilia fedha za tele kwa tele ambapo mwezi Machi 2017 Halmashauri imepokea Tshs 33,985,000.
Mwenyekiti wa Bodi akizungumzia utendaji kazi wa Bodi hiyo alisema ilikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha pale ilipohitaji kufanya ziara mbalimbali ndani ya Wilaya, malalamiko ya Wananchi kuhusiana na ukosefu wa Dawa katika Vituo vya huduma za Afya, Watumishi kukaa kwenye kituo kimoja kwa muda mrefu, na upungufu wa watumishi wa Sekta ya Afya.
Tangazo la nafasi za Wajumbe wa Bodi ya Afya litatolewa hivi karibuni.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM