Mkuu wa Wilaya ua Longido Mh.Frank James Mwaisumbe leo tarehe 15/07/2019 amefungua rasmi mafunzo ya uboreshaji wa daftali la kudumu la wapiga kura kwa waandishi wasaidizi na BVR operator ngazi ya kituo.
Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido .
DC mwaisumbe amewaasa wanasemina kuwa waamiifu na kutumia lugha nzuri wakat wote wa zoezi aidha amewataka wanasemima hao pindi zoezi litakapoanza watunze mashine hizo kwani zimenunuliwa kwa pesa nyingi na ndizo zitakazo tumika Tanzania nzima kwa ajili ya zoezi la uboreshaji wa daftali la wapiga kura.
Afisa Mwandikishaji jimbo la Longido Jumaa Mhina akiwaongoza wanasemina kura kiapo cha kutunza siri na kujitoa kwenye chama cha siasa.
Afisa Mwandikishaji jimbo la Longido ndugu Jumaa Mhina akiwaasa waandishi wasaidizi na BVR kit operator wakati wa mafunzo hayo.
Waandishi wasaidizi wa vituo na BVR kit operator wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali za uboreshaji wa daftali la kudumu la waliga kura.
Afisa Tehama(W) Bi Zaina Mzee akiwasilisha mada ya mfumo wa VRS(Voter Registration System) wakati wa mafunzo ya uboreshaji wa daftali la kudumu la wapiga kura.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM