Na Happiness Nselu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Bw. Nassoro Shamzigwa, amewaaga wanamichezo wa halmashauri hiyo wanaosafiri kuelekea mkoani Tanga kushiriki Michezo ya Watumishi wa Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA).
Akizungumza ofisini kwake kabla ya safari, Bw. Shamwigwa aliwataka wachezaji hao kwenda kushindana kwa nguvu huku wakilinda nidhamu na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
“Twende tukashindane, lakini tulinde nidhamu yetu. Sheria, kanuni na taratibu za utumishi zipo pale pale. Tuitangaze Longido, vivutio vyetu na utalii wetu,” alisema Mkurugenzi
Ameeleza kuwa michezo siyo tu burudani, bali pia ni afya na husaidia watumishi kuchangamana, kujenga mshikamano, na kubadilishana mawazo.
“Michezo ya SHIMISEMITA inatukutanisha watumishi wa serikali za mitaa kutoka nchi nzima. Kila mmoja anapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa mwenzake
mwalimu kwa mwalimu, daktari kwa daktari. Mkirejea nyumbani, nataka muwe wapya katika utendaji kazi,” aliongeza.
Michezo ya SHIMISEMITA mwaka huu inafanyika mkoani Tanga, ikihusisha mashindano mbalimbali yanayoshirikisha halmashauri kutoka maeneo yote ya Tanzania Bara.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.