Halmashauri ya Longido leo tarehe 02/10/2018 imeanza zoezi la kuhuisha fedha za Mpango wa Kunusuru kaya Masikini zinazotolewa na serikali kupitia mradi wa TASAF awamu ya III kwa wanufaika wa Mpango huo.
Afisa msimamizi wa zoezi hilo kutoka halmashauri Reginald Joseph Lyakurwa akizungumza wakati wa zoezi hilo amesema tumejipanga kutumia muda mfupi kabla ya kugawa fedha kwa lengo la kuwakumbusha wanufaika wa mpango kutumia fedha hizo kutokana na masharti ya TASAF.
Lyakurwa amefafanua kuwa kuna baadhi ya wanufaika wanashindwa kutekeleza masharti ya matumizi ya fedha hizo ikiwemo kuwahudumia watoto wanaosoma, kuwapeleka watoto kliniki pamoja na kuhudumia familia na badala yake wanatumia fedha hizo kwenye ulevi.
"Inatulazimu kuwakumbusha wasimamizi hawa wa kaya kutumia fedha hizo kutunza familia kwa kuwa imeonekana baadhi yao wakipata hela wanaishia kwenye pombe na kusababisha familia kuendelea kuteseka" amesema Lyakurwa.
Lyakurwa ameongeza kuwa mafunzo tutakayoendelea kuyatoa pamoja na ufuatiliaji wa karibu wa wanufaika hao yatasaidia kutatua changamoto hiyo kuliko kukaa kimya kuwaacha bila kuwakumbusha.
Hata hivyo wasimamizi wa kaya hizo waliofika kupokea ruzuku hizo wanajivunia kuwa mradi huu umefanya afya zao kuboreka na watoto wao kupata elimu ya uhakika.
Wameongeza kuwa kwa sasa makali ya gharama za matibabu pia imepungua kwani wana Bima za afya zinazowasaidia kupata matibabu na wategemezi wao bila shida yoyote na wanaomba mradi huu uendelee.
Naye mratibu wa TASAF halmashauri ya Longido Lobulu S.Saruni amesema kuwa kwa sasa wanalipa awamu ya nne tangu mradi huo kuanza na awamu hii wamelipa jumla ya shilingi milioni 184,608,000/= kwa kaya 5,641 kwenye vijiji 27 ndani ya halmashauri ya Longido.Vijiji vilivyonufaika na mpango ni Eleng'atadapas,Olchoroonyokie,Sokon,Kimwat,Mairowa,Ngoswaki,Sinonik,Kiserian,Magadini,Meirugoi,Alaililai,UchangitSaput,Irkaswa,Kamwanga,Kitendeni,MataleB,MataleA,Lesing'ita,Mundarara,Orgira,Namanga,Elerai,Lerang'wa,Olmolog,Longido,Orbomba na Ngereyani.
Lobulu amesema kuwa licha ya kuwa fedha hizo zinawasaidi wananchi hao lakini bado kuna changamoto ya baadhi ya wanakaya kushindwa kutimiza masharti ya TASAFj ambo ambalo linasababisha mwana kaya kukatwa kiasi cha fedha.
Hata hivyo Lobulu amesema kuwa kupitia maafisa wa halmashauri wanaokwenda kusimamia zoezi la ulipaji wa fedha kuhakikisha wanatoa mafunzo ya kuwakumbusha wanufaika hao kutumia fedha hizo kulingana na masharti ya TASAF.
Aidha amewataka wananchi wote wanaonufaika na Mpango kutumia fedha hizo vizuri pamoja na kutunza vitambulisho vyao vya TASAF na kuepuka kutuma mtu wa kumchukulia fedha jambo ambalo haliruhusiwi na linasababisha fedha kurudishwa.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM