Halmashauri ya wilaya ya longido leo tarehe 14.03.2019 wamefanya kikao katika ukumbi wa Halmashauri na kuweka mikakati ya kuhakikisha unyanyasaji wa wanawake na watoto wadogo unakomeshwa. Unyasaji huo ni pamoja na ubakaji,ulawiti kwa watoto wadogo hasa maeneo ya Namanga ,mimba mashuleni kwa watoto wa kike ,ukeketaji hasa kwa watoto wa kike,ndoa za utotoni ,unyasaji wa kisaikolojia,uhuru wa kushiriki kutoa mawazo pamoja na ukwepaji wa majukukumu,washiriki wa mikakati hiyo ni wakuu wa idara ya afya ,ustawi wa jamii,maendele ya jamii,jeshi la polisi ,wanasheria ,watendaji wa vijiji kadhaa pamoja wenyeviti wa vijiji,katika semina hiyo imeelezwa kwamba kuna changamoto nyingi sana katika utokomezaji wa ukatili wa kijinsia hasa ya mimba mashuleni ,ukeketaji,ulawiti na ubakaji,changamoto hizo ni :-
1.kutokuwepo kwa ushirikiano wa kutosha kati ya mwathirika wa tukio na vyombo vya dola
2.wazazi kutotoa ushirikiano wa kutosha katika swala zima la unyanysaji wa watoto
3.uwepo wa mrundika wa kabila moja kwenye uongozi kuanzia ngazi ya kata hadi vitongoji,hii inafanya wao wenyewe kuelewana wao kwa wao bila kumfikisha mtuhumiwa kwenye vyombo vya dola.
4.Ukosefu wa elimu katika jamii hasa kuhusu swala la ukeketaji ,jamii hii ya kimasai hawajui kabisa madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike.
Kutokana vitendo hii viovu ambayo waathirika wengi ni watoto wa kike na watoto wadogo serikali imejipanga kuhakikisha wanaeneza elimu ya nyumba kwa nyumba pamoja na hatua kali za kisheria zina chukuliuwa kwa mtu yeyote atakaebainika kuhusika na ukatili huu wa kijinsia.Pili kuhakikisha kwamba nguvu kazi (task force)katika jamii pamoja na kuwepo kwa wataalam mbalimbali katika jamii ili kuhakikisha mambo haya maovu yanatokomezwa,tatu jamii itambue kwamba unyanyasaji wa kijinsia hasa kwa watoto husababisha madhara mengi kwa watoto ikiwemo mtoto kukosa kujiamini,kuwa na msongo wa mawazo pamoja na maambuziki ya magonjwa mbalimbali hasa UKIMWI.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM