Mkutano wa Baraza la madiwani umefanyika leo tarehe 12-11-2019 katika ukumbi wa halmashauri ya Longido JK Nyerere ikiwa na agenda mbalimbali ikiwemo uwasilishaji wa taarifa mbalimbali za kamati ya kudumu za Halmashauri kwa kipindi cha Julai mpaka Septemba 2019, mkupitia maazimio ya mkutano uliopita , mapendekezo ya wajumbe wa kamati ya mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo (CDCF) na maswali yapapo kwa papo kwa mkurugenzi na Mhe mwenyekiti.
Mkutano huo umehudhuriwa na waheshimiwa madiwani kutoka katika kata takribani 18 wa wilaya ya Longido, wataalamu kutoka katika idara na vitengo mbalimbali vya Halmashauri na wadau kutoka katika asasi mbalimbali.
Moja ya maswali ambayo yaliulizwa kueleka kwa mwenyeki wa mkutano huo ni changamoto ya uhaba wa mabwawa ya kunyweshea Wanyama kiasi cha kufanya Wanyama kukosa maeneo ya kupata maji na kuamua kusogelea kwenye makazi ya wananchi na kuatarisha usalama wa wananchi.
Pia wajumbe waliwasilisha taarifa za utekelezaji wa kazi za kamati mbalimbali za kudumu zikiwemo kamati shirikishi ya kuthibiti ukimwi, kamati ya elimu afya na maji,kamati ya uchumi ujenzi na mazingira na mwisho ni kamati ya fedha utawala na mipango.
Vilevile mkutano ulihudhuriwa na katibu tawala wilaya Ndugu Toba Nguvila akimwakilisha Mkuu wa wilaya Ndugu James Frank alitoa shukrani nyingi kwa madiwani wote wa baraza hilo na kuwasisitaza wajumbe kwenye suala zima la usalama wa wananchi wa Longido pamoja na mali zao hasa ukizingatia wilaya yetu ipo mpakani.
Pia alizungumzia suala zima la mfuko wa Bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa (iCHF) na kuwataka waheshimiwa madiwani kuwahamasisha wananchi kujiunga kwenye mfuko huo ili wananchi waweze kupata nafuu ya huduma ya afya pale tu wanapohitaji kwani kwa sasa bila bima hiyo gharama ni kubwa ukizingatia na hali ya sasa.
Mwisho mwenyekiti wa kikao Mhe Diwani wa kata ya Sinya ndugu Sabore Molloimet alifunga mkutano na kuwataka waheshimiwa madiwani kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano, pia kuwashukuru wajumbe wote kwa uchangiaji wa maoni na ushauri katika kipindi chote cha mkutano.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM