Katibu mkuu ofisi ya Raisi tawala za mikoa na serikali za mitaa Tamisemi Mhandisi.Joseph Nyamhanga akiambatana na katibu tawala mkoa Arusha na secretariati ya mkoa leo tarehe 13-09-2019 akiwa katika halmashauri ya wilaya ya Longido amefanya ziara ya kutembelea na kujionea miradi mbalimbali ya maendeleo yaliyopo wilayani .Mhandisi Nyamhanga ametembelea kiwanda kidogo cha mikate kinacho julikana kwa jina la BLESSING BEKARY, ambapo waliweza kumueleza Katibu mkuu TAMISEMI kuwa walianza mradi wao kwa kiwango cha fedha taslim milioni kumi walio chukua kama mkopo kutoka ofisi ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya Longido akieleza afisa maendeleo ya Jamii Bi. Grace kuwa waliweza kutoa zaidi ya milioni mia moja thelathini kwa ajili ya vikundi ikiwa asilimia 6% ni kwa ajili ya wakina mama na kikundi cha vijana 2% pamoja na walemavu 2%, Kikundi hichi kilinufaika kwa ujio wa kiongozi huyo kwani aliweza kununua mikate miamoja ambayo aliitoa zawadi pamoja na mbuzi kwa kituo cha watoto yatima Namanga. Pia alitembelea vituo vya afya cha Eworendeke pamoja na kutembelea miradi inayoendelea ikiwemo hospitali ya wilaya, barabara ya kiwango cha lamiyenye urefu wa kilomita moja kutoka kituo cha polisi Longido hadi zahanati ya Longido na kutembelea kikundi cha walemavu kinachojulikana kwa jina la OSILIGI kilichopo kata ya kimokouwa wilayani Longido katibu mkuu TAMISEMI aliweza kuwaunga mkono kwa kununua mbuzi moja wapo wa mbuzi wanao nenepeshwa na kikundi hicho kwa shilingi Laki moja (100,000/=)
Katika ziara hiyo katibu mkuu ndugu Mhandisi Joseph Nyamhanga alipata fursa ya kufanya kikao kifupi na watumishi wa Halmashauri ya wilaya wakiwemo wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri, taasisi za kiserikali tarura, maafisa taarafa na watendaji wa kata.
Katika kikao hicho mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Longido Ndugu Jumaa Mhina alipata fursa ya kutoa taarifa ya miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo katika halmashauri pamoja na miradi mikakati takribani kumi ambayo ikikamilika itaongeza mapato ya halmashauri kufikia takribani bilioni sabini kwa mwaka.
Pia mkurugenzi mtendaji ndugu Jumaa Mhina alisema Halmashauri imepiga hatua kubwa kwenye sekta mbalimbali ukilinganisha na miaka iliyopita mfano kwenye ukusanyaji mapato umeongezeka kutoka tsh milioni 400 mpaka tsh bilioni 2, sekta ya elimu imekuwa ya pili kimkoa na ya tano kitaifa kwenye mitihani ya kidato cha pili mwaka jana na watumishi wengi waliokuwa hawajathibitishwa kwenye idara na vitengo vyao sasa wamethibitishwa. Pia katika kikao hicho katibu tawala wilaya ndugu Toba Nguvila alielezea changamoto ya gari la kufanyia patroo ndani ya Wilaya ya Longido yenye ukubwa wa kilomita 320 katibu mkuu TAMISEMI alijibu kuwa atalifanyia kazi kwa haraka kwani hili ni eneo la mpakani hivyo ni muhimu kuwa na gari hilo ili kulinda maliza raia na utorohwaji wa mifugo kuingia nchi jirani.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM