Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2018 Ndg. Charles.F.Kabeho alitembelea miradi sita ya maendeleo tarehe 15/09/2018 . Baadhi ya miradi imewekwa jiwe la msingi, kufunguliwa , kutembelewa na kuzinduliwa.Miradi hiyo kwa ujumla imegharimu serikali takriban Tsh. 2,892,288,316.00.
Miradi hiyo iliyozinduliwa na kuwekewa jiwe la Msingi na kutembelewa ipo katika sekta mbalimbali za utawala bora,Elimu,Afya,Maendeleo ya jamii,Kilimo na Maji.
Ndg .kabeho aliweka jiwe la msingi katika ofisi ya kijiji ya Noondoto ujenzi uliogharimu kiasi cha Tsh.47,000,000/-.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa pia amezindua madarasa matatu katika shule ya msingi kitumbeine ujenzi uliogharimu kiasi cha Tsh.53,450,000/-
Vile vile kiongozi wa mbio za mwenge ameweka jiwe la msingi katika kituo cha afya Ketumbeine, mradi uliogharimia Tsh. 600,000,000/-
Ndg.Kabeho pia amezindua mradi wa maji kijiji cha mairowa wenye thamani ya Tsh.1,903,998,800.
Hata hivyo Kabeho ameendelea kuifurahia miradi ya Longido na kuitolea mfano hata wakati wa kukabidhi mwenge huo kwa halmashauri ya Arusha.
Amesema nimeona ujenzi wa madarasa matatu yenye viwango yamejengwa kwa gharama ndogo ya milioni 53,000,000/- na mazingira yake ni magumu hata kusafirisha vifaa ,sasa nakuja huko nikiwa na picha ya Longido katika kutekeleza miradi ya maendeleo alimaliza ndg.Kabehe.
Ndg. Charles pia alitoa ujumbe wa mwenge uliosisitiza, wananchi katika sekta ya elimu kuendelea kutekeleza majukumu yao ya msingi kwa watoto wao. Serikali imeondoa michango na ada kwa shule za msingi na sekondari mpaka kidato cha nne. Wazazi wanapaswa kuwapa wanafunzi, sare za shule, madaftari, kalamu viatu na kuwapatia chakula wanapokuwa shuleni.
Ndg. Kabeho amesema serikali inaendelea na mapambano dhidi ya ukimwi, imeendelea kusisitiza watu kujua afya zao. Mpango wa sasa ni kuomba wanaume kujitokeza kupima na kupata ushauri nasaha, wanaume wamekuwa wagumu mno kujitokeza kupima.
Ndg. Kabeho amesema serikali inaendelea na mapambano dhidi ya rushwa, rushwa ni adui wa haki ni vizuri kutoa taarifa kwa vyombo husika au kutumia namba 113 ambayo ni bure kwa mitandao yote. Ndg. Kabeho amesema serikali inaendelea na mapambano dhidi ya malaria serikali inatoa vyandarua kwa kinamama wajawazito. Nivyema kujua matumizi sahihi ya vyandarua hivi.
Ndg kabeho amesema serikali inaendelea na mapambano dhidi ya dawa za kulevya, ni vizuri wananchi wakaacha matumizi mabaya ya dawa za kulevya kwa sababu yanaongeza vitendo vya uhalifu na kurudisha maendeleo nyuma
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM