Na:Saumu Kweka
Approved By Joseph Peter Mkumbwa. ICTO
Mwishoni mwa wiki hii kutakuwa na uzinduzi rasmi wa burudani ya kukata na shoka ya mchezo wa mpira wa miguu kwa vijana katika viwanja vya michezo vya Polisi Longido/Old Trafod.
Ligi hiyo itaanza rasmi jumapili ya tarehe 24,ikizikutanisha timu za Longido Worriours dhidi ya Kitumbeine Fc katika viwanja vya Polisi mida ya saa 10 alasiri.
Lengo kuu la ligi hiyo ikiwa ni kuwaweka Vijana pamoja,kuangalia vipaji vya vijana na kuleta burudani kwa jamii.Huku wachezaji wakitahadharishwa kufuata kanuni zote 17 za Ligi,ikiwa ni pamoja na kila timu kuwa na jezi zao,kila timu kuwa na daktari ,pia timu itakayosababisha vurugu itatozwa faini ya shilingi 100,000 kama ilifafanuliwa kwenye kanuni za TFF nk.
Timu zitakazoshiriki katika Ligi hiyo ni pamoja na Longido Warriours,Namanga Veteran,Orbomba FC,Namanga Sports,Longido Veteran ,Vijana Stars ya Longido na Kitumbeine FC.
Pia viwanja vitakavyotumika katika Ligi hiyo ya Mkuu wa Wilaya ni vya Polisi Longido /Old Trafod,Namanga shule ya msingi,Longido Sekondari,na Kitumbeine.Huku ligi hiyo ikitarajia kukamilika Disemba 6 mwaka huu.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM