Na:Saumu Kweka
Approved By Joseph Peter Mkumbwa. ICTO
Ligi ya Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa Daniel Chongolo,imeanza rasmi kwa kufunguliwa rasmi na pambano lililozikutanisha timu za Longido Worriours dhidi ya Kitumbeine Fc.
Mtanange huo wa aina yake ulionekana kuwavutia mashabiki wengi ulichezeka vyema huku timu ya Longido Worriours ikiibuka washindi wa pambano hilo baada ya kutandika timu ya Kitumbeine Fc goli 2-0.
Mechi hiyo ya kirafiki ilipigwa katika viwanja vya Polisi Longido maarufu kama Old Trafod huku timu zote zikicheza kwa nidhamu ya hali ya juu na kufuata kanuni zote 17 za TFF .Lakini kwa bahati mbaya timu zote mbili zilipata idadi ya kadi 6 za njano,Longido Worriours idadi ya kadi 3,na Kitumbeine Fc idadi ya kadi 3 za njano.Ikiwa hakuna timu yoyote iliyoripotiwa mchezaji wake kupewa kadi nyekundu.
Mechi nyingine itapigwa Septemba 27,siku ya Jumatano saa 10 alasiri katika viwanja vya shule ya Sekondari Longido itakayozikutanisha timu za Longido Veteran dhidi ya Vijana Stars
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM