Halmashauri ya Wilaya ya Longido kupitia Idara ya Elimu sekondari imejidhatiti kuhakikisha wanafunzi watakaomaliza kidato cha sita kuendelea na elimu ya juu.
Amebainisha hayo Afisa elimu sekondari Wilaya ya Longido Gerson Mtera mapema leo ambapo ameeleza kuwa wanafunzi watakao hitimu kidato cha sita hawana mashaka nao kwani alama walizokuwa wakipata kwenye mitihani ya nyuma pamoja na moko imewaakikishia ushindi.
Gerson amebainisha kuwa kwa shule zinazotoa elimu ya High-Level ambazo ni Longido sekondari (201) na Engikareti (15) mwaka 2018 hawakuwa na division 4 wala 0 lakini pia katika mitihani iliyokuwa ikifanyika ya shule kwa shule na mazoezi mbalimbali, mitihani ya mara kwa mara pamoja na masomo ya ziada yaliyotolewa wamekuwa wakifanya vizuri.
Aidha ufaulu huo utaambatana na semina iliyotolewa shuleni hapo na wataalamu April 16, 2019, mazungumzo kati ya Idara ya elimu, Mkurugenzi, Mkuu wa Wilaya, Katibu mwenezi Taifa pamoja na wadau mbalimbali wa elimu dhidi ya wanafuzi hao.
Hata hivyo wanafunzi hao wamekwishapewa ofa ya kupata mkopo wa 100% watakaopata division one na two vilevile wamekwisha patiwa semina ya jinzi na namna ya kujaza form za kuomba mkopo kupitia kwa Naibu Waziri wa Elimu Mhe. William Ole Nasha.
Gerson amewataka wanafunzi, wasimamizi, walimu ,wazazi na walezi, pamoja na wadau mabalimbali wa elimu Wilayani Longido kwamba kila mmoja atomize wajibu wake bila kukiuka sheria na taratibu za kimtihani.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM