Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Ndg. Loota Sannrei ameitaka Halmashauri ya Longido kuhakikisha inatenga siku maalumu ya kuwa inakutana na Wananchi ili kusikiliza kero huku shughuli hiyo ikiambatana na utatuzi wa hizo kero.
Ameyasema hayo jioni ya Juni 24, 2019 baada ya kumaliza ziara yake ndani ya Wilaya hiyo ambapo ametembelea na kukagua Miradi ipatayo minne ili kujiridhisha kama Ilani ya CCM inatekelezwa huku akijidhirisha na kiwango pamoja na kasi ya utekelezaji huo kwa zaidi ya asilimia 90%.
Ndg. Loota Sannrei amesema kuwa wamepata Wilaya ambayo ni kipenzi cha watu kwani katika Wilaya zote alizotembelea hajaona utekelezaji wa kiwango kama cha Longido kwani Miradi inaenda vizuri kwa wakati na yenye viwango. Pia ameongeza kuwa hii ndio maana halisi ya kusema CCM mpya na Tanzania mpya.
Awali akijibu kero ya Madiwani iliyokuwa inalenga kuhakikisha Mradi wa maji unawafaidisha wanalongido ambao umeonekana mabomba yake kupasuka huku mengine yakikatwa na Wilaya jirani ya Siha jambo linalopelekea kushindwa kuhudumia kama ilivyotarajiwa, Ndg. Sannrei amewatoa wasiwasi kuwa tarehe juni 29, 2019 atakutana na wakuu wa Wlaya mbili yaani Siha pamoja na Longido wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakae kwa pamoja na kupata majawabu ya changamoto hiyo.
Ameendelea kusema kuwa Viongozi wa CCM wanaoitwa na kushindwa kufika bila ya kutoa sababu siku zao zinahesabika kwani CCM haiwezi kuwavumilia Viongozi kama hao ambao hawahudhulii vikao hivyo vinavolenga kuboresha chama hicho. Amewataka , Mwenyekiti ,Mkurugenzi, katibu kuhakikisha wanakuwa na majina ya waliohudhulia vikao mara kwa mara ili mwisho wa siku wawatambue wanaofaa mapema.
Kwa upande wake M/Kiti wa CWT Mkoa wa Arusha Yasmin Bachu amesema wao kama wanawake wanaandaa kongamano la kumpongeza Mhe. Magufuli Rais wa Tanzania ambalo litafanyika julai 7, 2019 katika viwanja vya Shekh Amri Abed Karume kwa lengo la kulekebisha Kupunguza na kutatua yote yanayotatiza maendeleo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Frank James Mwaisumbe amesema kuwa wanafanya kazi kwa niaba ya Wanalongido usiku na mchana ili kuhakikisha yote yanayoelekezwa yanatekelezwa kwa wakiti na kwa viwango stahiki.
Aidha amesema Miradi minne iliyotembelewa ikiwemo Kiwanda cha Nyama, Soko la Mifugo n.k. ni miradi mikubwa itakayotatua changamoto za ajira, mzunguko wa biashara ndani na nje ya nchi. Pia ametoa ufafanuzi kuwa Miradi hiyo imekwishaanza kuwanufaisha kwa kutolea mfano Mradi wa maji ambayo umeshaanza kusambazwa ndani ya Longido na yanatoka mabombani.
Ametoa changamoto ya Mradi huo kuwa ni mabomba kupasuka, baadhi ya watu hawana licha ya kuwa yamesambazwa, lakini wakati huo amekwisha zungumza na wahusika wa ujenzi wa Mradi huo wakiwemo AUWASA kuhakikisha wanabadilisha mabomba hayo.
Mhe. Mwaisumbe amesema Serikali imekwisha tenga Tsh. Billion 2.5 za kuhakikisha Mradi huo unasambaza maji ndani vijiji, kata na maeneo yote mpaka kata ya Namanga iliyoko mpakani mwa Kenya. Huku akisema ni ishara tosha ya kunyakua viti vyote vya Maniwani na Wanyeviti mwaka huu na mwaka ujao.
Sabore Molloimet Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri Longido amesema kuwa Miradi yote hito iliyotembelewa na ambayo haijatembelewa, iliyowekewa mawe ya msingi na kuzinduliwa ni ishara tosha ya kuonesha Longido ni CCM kwani kwa asilimia kubwa viongozi ni wa CCM na ndio maana shughuli zinaenda kama inavyopangwa.
Vilevile amesema kuwa kutokana na kukosoana na kushauriana kupitia vikao na mikutano ambavyo wamekuwa wakifanya mara kwa mara kwa mambo mbalimbali ya kimaendeleo Longido sasa inaenda kwa kasi kubwa na wanakuja kuwazidi Wilaya nyingine hatakama ni kongwe.
Ameendelea kusema kuwa shukrani na pongezi kubwa zimwendee Dk. John Magufuli kwa kuwapa kipaumbela na kuwamwagia pesa nyingi za maendeleo ndani ya Longido za Ujenzi wa Miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Hospitali kubwa ya Wilaya, Mradi mkubwa wa Maji n.k.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM