• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Miundombinu, Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mjjini
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Utawala na Usimamizi wa Rasimamli Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Utalii
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Leseni
    • Huduma za Utalii
    • Huduma za Mapato
    • Huduma zetu Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati ya Maadili ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Barua pepe za Idara na Vitengo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Kituo cha habari
      • Maktaba ya Picha
      • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
  • Vivutio
    • Mbuga
    • Ziwa

LONGIDO YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA MAFANIKIO MAKUBWA

Posted on: June 17th, 2025

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yamefanyika kwa mafanikio makubwa katika viwanja vya Shule ya Msingi Namanga wilayani Longido, yakihudhuriwa na viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo, wazazi na wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido, Bi. Rahma Kondo, aliwapongeza wadau wote wanaojihusisha na ustawi wa watoto kwa kushiriki kikamilifu katika maandalizi na utekelezaji wa maadhimisho hayo muhimu.“Napenda kutoa shukrani za dhati kwa wadau wote wanaoshughulika na masuala ya watoto kwa moyo wa kujitolea, pamoja na kushiriki kikamilifu katika maadhimisho haya.

 

Siku ya Mtoto wa Afrika ni kumbukumbu ya kipekee inayotukumbusha sisi wazazi na walezi juu ya wajibu wetu wa kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira salama na yenye staha,” alisema Bi. Rahma.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Bw. Rajab Mmbunda alieleza kuwa maadhimisho haya ni jukwaa muhimu la kuwakumbusha wananchi kuhusu haki za msingi za watoto, ikiwa ni pamoja na haki ya kupata elimu, afya, ulinzi, na malezi bora.

Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ilikuwa: “Haki ya Mtoto: Tulipotoka, Tulipo na Tuendako,”ikilenga kutathmini hatua zilizopigwa katika kulinda haki za watoto, changamoto zilizopo na mikakati ya kuimarisha ustawi wa watoto barani Afrika.

Mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yalijitokeza kushiriki na kutoa mchango wao mkubwa katika tukio hilo. Miongoni mwa mashirika hayo ni ACE Africa, CORDS Tembo, Compassion International, na MPDI, ambayo yameendelea kuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya mtoto katika wilaya ya Longido kupitia miradi mbalimbali ya elimu, afya, lishe na ulinzi wa mtoto.Maadhimisho hayo yalipambwa na nyimbo,maigizo ngonjera kutoka kwa watoto na wadau mbalimbali.

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA June 13, 2025
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WA UMMA April 12, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA May 15, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA June 25, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • View All

Video

MKUU WA WILAYA YA LONGIDO AUNGANA NA RC KIHONGOSI KWENYE JOGGING YA TANZANIA SAMIA CONNECT
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.