• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Miundombinu, Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mjjini
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Utawala na Usimamizi wa Rasimamli Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Utalii
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Leseni
    • Huduma za Utalii
    • Huduma za Mapato
    • Huduma zetu Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati ya Maadili ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Barua pepe za Idara na Vitengo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Kituo cha habari
      • Maktaba ya Picha
      • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
  • Vivutio
    • Mbuga
    • Ziwa

LONGIDO YAAGA MADIWANI WAKE KWA HESHIMA, YASIFIA UONGOZI WAO WA HEKIMA NA BUSARA

Posted on: June 20th, 2025

Na Happiness Nselu – Longido

Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido umeonyesha kuthamini mchango wa viongozi wa Baraza la Madiwani waliomaliza muda wao, kupitia kikao kifupi cha kuagana kilichofanyika leo tarehe 20 juni 2025 katika ukumbi mdogo wa halmashauri hiyo.

Katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Simoni Oitesoi na Makamu Mwenyekiti Mhe. Peter Lekanet waliowakilisha Madiwani wengine, walipongezwa kwa uongozi wao wa hekima, busara na uwajibikaji uliosaidia kuleta mageuzi makubwa katika Halmashauri hiyo.

Kwa kipindi cha uongozi wao kuanzia mwaka 2020 hadi 2025, Halmashauri hiyo imefanikiwa kuongeza mapato ya ndani kutoka shilingi bilioni 1.5 hadi kufikia shilingi bilioni 5 kwa mwaka mchango ambao Menejimenti ya Halmashauri umeutambua kama wa kihistoria.

Akizungumza kwa niaba ya Madiwani wenzake, Mhe. Oitesoi alisema kuwa mafanikio hayo yamechangiwa na ushirikiano wa karibu baina ya Baraza la Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri. Alisisitiza kuwa wamefanya kazi kwa mshikamano na kuweka mbele maslahi ya wananchi wa Wilaya ya Longido.

Makamu Mwenyekiti Mhe. Peter Lekanet, kwa upande wake, alieleza kuwa uongozi wao ulilenga kuimarisha misingi ya amani, uwajibikaji na utulivu kazini ili kuwezesha watumishi kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Nae, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Bw. Nassoro Shemzigwa, alitoa salamu za shukrani kwa niaba ya menejimenti, akiwahakikishia viongozi hao kuwa kazi waliyoifanya imeacha alama isiyofutika katika historia ya halmashauri hiyo.

Akizungumzia kuondoka kwao, Bw. Shemzigwa alisema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi ya mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025, na kwamba menejimenti inaichukulia kama mapumziko ya muda mfupi kwa viongozi hao.

“Kwa kweli tunaamini kwamba huu si mwisho, bali ni mapumziko ya muda. Ni matumaini yetu kama Menejimenti kwamba tutawaona tena, tukiendelea kushirikiana katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Halmashauri yetu,” alisema kwa matumaini.

Kwa ujumla, kikao hicho kimeacha taswira chanya ya mshikamano kati ya watumishi na viongozi waliomaliza muda wao, hali inayowapa matumaini wananchi wa Wilaya ya Longido juu ya mustakabali wa maendeleo ya wilaya yao.



Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA June 13, 2025
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WA UMMA April 12, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA May 15, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA June 25, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • View All

Video

MKUU WA WILAYA YA LONGIDO AUNGANA NA RC KIHONGOSI KWENYE JOGGING YA TANZANIA SAMIA CONNECT
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.