Halmashauri ya Wilaya ya Longido chini ya Mkurugenzi Mtendaji Ndug. Jumaa Mhina kupitia Idara ya Utumishi imeweka misingi ya kuhakikisha wanafunzi wanapata haki stahiki shuleni kwa kutoa ajira za muda za Walimu kumi na watano(15).
Akitoa taarifa hiyo ya kwa maandishi Afisa utumishi msaidizi Stephen Mbombe Ofisini leo julai 11, 2019 amesema kuwa tayali Walimu 15 wa wamekwisha pewa ajira za muda na kwa kuhakikisha wanawanoa vijana wa Longido kielimu na kuwa mishahara yao imekwishaanza kutoka.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa wameangalia vigezo stahiki kulingana na mahitaji ya Walimu Wilaya iliokuwa nayo yaani viwango vya Elimu, masomo husika atakayofundisha Mwalimu kulingana na uhitaji wa Shule husika.
Taarifa ya Mbombe imewataja walimui hao kuwa ni Sospeter Machuwa Say alietoka Chuo cha Uwalimu Korogwe mwenye Stashahada ya Elimu daraja la (IIIB) na atafanya kazi ya kufundisha katika Shule ya Sekondari Longido, Catherine Lucas Masanyi kutoka Chuo kikuu Dodoma mwenye Shahada ya Elimu ya Sayansi na Kompyuta kwa daraja la (IIIC), Jestina Esau Mluyo mwenye Astashahada ya Elimu ya Sekondari kwa daraja la (IIIB) na atakuwa akifanya kazi hiyo katika Shule ya Sekondari Tingatinga.
Catherine Kastuli mwenye Shahada ya Sayansi ya Elimu kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam aiwa na daraja la (IIIC) na atafanya kazi Shule ya Sekondari ya Enduiment, vilevile Letain Kurenia Mollel kutoka Dar es salaam mwenye Shahada ya Sayanzi ya Elimu kwa daraja la (IIIC) na atakuwa shule ya Lekule ya sekondari, Adela Filbet Obandia kutoka Chuo kikuu cha Sauti akiwa na Shahada ya Elimu ya masomo ya Sanaa na atakuwa Longido Sekondari, Boniface Malley kutoka Chuo cha Tabora Astashahada ya Elimu na atakuwa akifanya kazi shule ya Kimwati Sekondari pamoja na wengine waliopata ajira hizo.
Taarifa imeendelea kueleza kuwa Halmzashauri itaendelea kuhakikisha inatengeneza mazingira ya wanafunzi kufauru ili kuondoa changamoto zisizo za lazima.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM