• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Miundombinu, Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mjjini
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Utawala na Usimamizi wa Rasimamli Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Utalii
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Leseni
    • Huduma za Utalii
    • Huduma za Mapato
    • Huduma zetu Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati ya Maadili ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Barua pepe za Idara na Vitengo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Kituo cha habari
      • Maktaba ya Picha
      • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
  • Vivutio
    • Mbuga
    • Ziwa

LONGIDO YATOA VIPAJI KUUNDA TIMU YA MKOA KWENYE MASHINDANO YA UMISSETA

Posted on: June 6th, 2025

Baada ya kufanyika kwa mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya wilaya, Wilaya ya Longido imepata wanafunzi mahiri watakaoungana na wenzao kutoka wilaya nyingine kuunda timu ya Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kushiriki mashindano ya UMISSETA ngazi ya mkoa.

Mashindano hayo ya ngazi ya wilaya yalifanyika kwa siku kadhaa yakihusisha shule mbalimbali za sekondari kutoka maeneo yote ya Longido, ambapo wanafunzi walishindana katika michezo ya mpira wa miguu, netiboli, mpira wa wavu, riadha na mingineyo.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa wachezaji waliochaguliwa, Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Longido, Bi. Asha Kivaju, alisema kuwa uchaguzi huo umefanyika kwa kuzingatia vipaji, nidhamu na uwezo wa wachezaji kwa ujumla.“Tumeweza kupata vijana 120 waliothibitisha uwezo wao na sasa watawakilisha Longido katika timu ya mkoa. Hii ni fahari kubwa kwetu kama wilaya kuona mchango wetu unatambulika hadi ngazi ya juu,” alisema Bi. Asha.

Aidha, alitoa wito kwa wazazi, walimu na jamii kwa ujumla kuendelea kuwapa sapoti wanafunzi hao, kwani michezo ni sehemu muhimu ya kukuza vipaji, kujenga nidhamu, kuimarisha afya na kuleta fursa za maendeleo kwa vijana.Wakati huo huo, baadhi ya wanafunzi waliopata nafasi hiyo walieleza furaha yao kwa kuchaguliwa kuwakilisha mkoa na kuahidi kuitumia fursa hiyo vizuri kwa kuonyesha nidhamu, ushindani na uzalendo.


“Ni ndoto yangu siku moja kuvaa jezi ya timu ya taifa, na hii ni hatua muhimu kuelekea huko,” alisema Hassan Mohamed, mmoja wa wanafunzi waliochaguliwa.Mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa yanatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 9  mwezi huu katika viwanja vya shule ya Sekondari Ilboru  Arusha, ambapo timu ya mkoa itachaguliwa rasmi kwa ajili ya kuiwakilisha Kanda katika mashindano ya Taifa.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 08, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA ( LINARUDIWA ) October 10, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA October 19, 2024
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA LONGIDO AWATAKIA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA KILA LAHERI KWENYE MITIHANI YAO

    September 09, 2025
  • HUDUMA ZA UPASUAJI ZAANZA RASMI KITUO CHA AFYA EWORENDEKE - LONGIDO

    September 06, 2025
  • HUDUMA ZA UPASUAJI ZAANZA RASMI KITUO CHA AFYA EWORENDEKE - LONGIDO

    September 06, 2025
  • RC ARUSHA ATOA WITO WA AMANI NA UTULIVU LONGIDO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

    September 04, 2025
  • View All

Video

WASICHANA WA SHULE YA SEKONDARI LONGIDO WAPATIWA ELIMU YA HEDHI SALAMA NA MSAADA WA TAULO ZA KIKE
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.