Maafisa Uchaguzi Wasaidizi 69 ngazi ya Wilaya ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido wamehudhuria mafunzo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024. Mafunzo haya yamefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido kwa lengo la kuwaandaa maafisa hao katika kuendesha uchaguzi kwa ufanisi na kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa. Mafunzo hayo yanawahusisha mbinu bora za kusimamia mchakato wa upigaji kura, usimamizi wa vituo vya kupigia kura, pamoja na jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kutokea wakati wa uchaguzi.
Mafunzo hayo yameandaliwa ili kuhakikisha kuwa maafisa uchaguzi wasaidizi wanapata uelewa wa kina kuhusu taratibu na sheria zinazohusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024. Katika mafunzo haya, mada mbalimbali zimejadiliwa, ikiwa ni pamoja na:
Sheria na Kanuni za Uchaguzi, Maafisa walielimishwa juu ya sheria zinazohusiana na mchakato wa uchaguzi, ikiwa ni pamoja na haki na wajibu wa wapiga kura, wagombea, na wasimamizi wa uchaguzi.Utunzaji wa Vifaa vya Uchaguzi, Wamefundishwa jinsi ya kusimamia na kutunza vifaa vya uchaguzi, kama vile masanduku ya kura, karatasi za kupigia kura,ili kuhakikisha usalama na uadilifu wa zoezi zima.Usimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura, Maafisa hawa walifundishwa mbinu bora za kuandaa na kusimamia vituo vya kupigia kura, kuhakikisha kila kitu kinaenda kwa mpangilio na upigaji kura unafanyika kwa amani.
Kuepusha na Kukabiliana na Migogoro, Walielekezwa namna ya kushughulikia malalamiko, migogoro, au vitendo vya uvunjifu wa sheria vinavyoweza kutokea wakati wa uchaguzi, ili kuhakikisha zoezi linaendelea kwa amani na haki.Mafunzo haya ni sehemu muhimu ya maandalizi ya uchaguzi, yakilenga kuimarisha uadilifu na kuondoa changamoto zozote zinazoweza kutokea wakati wa mchakato wa uchaguzi. Maafisa hao wametakiwa kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa uaminifu ili kuhakikisha wananchi wanapata haki yao ya kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa kwa njia iliyo huru na ya haki.
"UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA SAUTI YA WANANCHI SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA".
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM