Shirika la maendeleo ya jamii HEIFER Tanzania International leo tarehe 30/6/2918 limekabidhi madume 70 aina ya boran kwa uongozi wa Wilaya ya Longido.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa madume hayo katibu Tawala wilaya ya longido ndg.Toba Nguvila aliipongeza sana shirika la HEIFER kwa kutambua hitaji kubwa la jamii kwani asilimia 95% ya wananchi wa longido wafugaji.
Aidha aliendelea kusema kuwa kwa wilaya ya viwanda ni imani yake sasa soko la kuchakata nyama litakapo kamilika litapata mifugo yenye afya na nyama ya kutosha itakayo kidhi mahitaji ya watu.
Nguvila aliwataka maafisa mifugo wa halmashauri wasimamie madume hayo na kuyafuatilia kuhakikisha lengo la mradi linatimia la kuwa na ng'ombe bora wa kisasa.
Naye kaimu mkurungenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya longido ndg.Gerson Mtera ametoa ombi kwa shirika la HEIFER kusaidia kupatikana kwa maji ya mifugo kwani kutokana na mvua zilizonyesha zimesababisha mabwawa matatu kupasuka na matokeo yake kusababisha upotevu wa maji yaliyokuwa yakitegemewa kwa ajili ya mifugo.
Lakini pia Mtera ameliomba shirika la HEIFER kufikisha mradi huu kwa vijiji vyote vya wilaya ya Longido.
Naye mratibu wa mradi ndg sayaeli amefafanua kuwa mradi huu unatekelezwa kwa muda wa miaka 5 na ulianza mwaka 2015 na utakamilika 2020
Aidha mradi huu unafanyika katika vijiji 8 vya tarafa ya Engarenaibor na Kitumbeine.
Nao wananchi wa vijiji hivyo wamelishukuru sana shirika la HEIFER na kuahidi kuyatunza madume hayo ili wapate ng'ombe bora katika vijiji vyao na kuweza kuyaboresha maisha yao.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM