Na Johnson Ismail
Approved By Joseph Peter Mkumbwa. ICTO
Sherehe ya Mahafali ya kidato cha nne yamefanyika hii leo shuleni kwa wahitimu 185 wavulana wakiwa 79 na wasichana 106,Wahitimu hao wana tarajia kuanza Mtihani wao wa mwisho Trh,30 mwishoni mwa mwezi huu.
Mahafali hayo yalihudhuriwa na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Longido Mh.Daniel Godfrey Chongolo,Pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Michael Lekule Laizer,Kaimu Mkurugenzi Dominck Ruhamvya,Katibu Tawala Toba Nguvira,Madiwani,Wakuu wa Idara,Katibu Tarafa,Mwenyekiti wa bodi ya shule,walimu wa shule mbalimbali,wazazi na Wageni waalikwa.
Mgeni Rasmi Mh.Chongolo amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao wawapo nyumbani na kuhakikisha wanaenenda katika njia nzuri kwani kuhitimu kidato cha nne sio mwisho wa elimu Pia amewaasa wanafunzi juu ya mimba shuleni na kusema serikali iko nyema kuhusiana na swala hili, amewataka wanafunzi kuachana na kutumia mitandao vibaya ili kuhakikisha wanafikia malengo mazuri .
Nao wanafunzi wamesema wamejipanga vyema kwa Mtihani na kuwahakikishia Waalimu na Wazazi matokeo mazuri huku wakiwashukuru walimu kwa kujitoa kwao kuwafundisha pasIpo kujali weekend ama siku ya mapumziko.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM