Maonyesho ya Kilimo yanaendelea kufana katika Viwanja vya nanenane vilivyopo Themi Jijini Arusha wakati yakielekea kileleni Agosti 8, 2018 yakiwa na kaulimbiu "Wekeza katika Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kwa maendeleo ya Viwanda."
Halmashauri ya Wilaya ya Longido inashiriki kwenye maonyesho hayo ikiwa na bidhaa mblimbali ikiwemo mazao ya Kilimo, Ufugaji na shughuli za wajasiriamali wanaopatikana ndani ya Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji Ndg Jumaa Mhina ametoa wito kwa Wananchi kutembelea banda la Longido kujionea bidhaa hizo.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM