Maendeleo ni namna ya kutoka hatua moja iliyo ya chini kwenda hatua nyingine ya juu kimafanikio. Ujenzi wa Miradi ya maendeleo ni swala mtambuka kwa maana halina mwisho na sababu kubwa ya kupelekea ujenzi wa Miradi ya maendeleo kutokuwa na mwisho ni kutokana na ongezeko la uhitaji wa huduma za kijamii, kisiasa na kiuchumi kila kuhitwapo leo.
Mbio za mwenge wa Uhuru ndio dhana kubwa ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania iliyojidhatiti katika uzinduzi ,ukaguzi na utembeleaji wa Miradi ya Maendeleo kama Viwanda, Barabara, Shule, Maji n.k. katika kila mwaka na kupitia Halmashauri mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya ya Longido mkoani Arusha ni miongoni mwa Halmashauri changa toka kuanzishwa kwake mwaka 2007 lakini imepiga hatua kubwa hasa katika ukusanyaji kodi, utekelezaji wa Miradi ya maendeleo kama miundombinu ya Maji, Barabara, umeme, ujenzi wa Vituo vya Afya kama Hospitali ya Wilaya, Soko la Madini, Kiwanda cha kusindika Nyama n.k.
Tarehe 07.06.2019 ni siku ya kipekee katika mwaka 2019 katika Wilaya ya Longido kwa kumbukumbu ya mbio za Mwenge wa Uhuru uliopita katika maeneo mbalimbali kwa uzinduzi, ukaguzi na utembeleaji wa Miradi mbalimbali iliyokwisha tekelezwa na inayoendelea kutekelezwa kwa kuweka Mawe ya Msingi, kuangalia namna utekelezaji unavyoendelea/kuendeshwa pamoja na kutoa ushauri na mapendekezo katika sehemu zinazohitaji maboresho.
Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Longido umetembea Kilomita 202.5, umepita katika Trafa mbili kati ya nne zilizopo ambazo ni Kitumbeine na Longido pia umekimbizwa Kata sita kati ya 18 na ulipita katiuka vijiji 10 kati ya 49 vya Wilaya ya Longido.s
Zoezi zima la uzinduzi, ukaguzi na utembeleaji wa Miradi limeanzia mnamo saa 4:00 asubuhi mara baada ya shughuli ya kuupokea Mwenge wa Uhuru lililoanza saa 2:30 asubuhi katika viwanja vya kata ya Gelai Merugoi vinavyo zitenganisha Wilaya mbili yaani Longido na Ngorongoro chini ya kiongozi mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali. Katika uzinduzi wa Miradi hiyo amegusia Sekta za Elimu, Maji, Uhifadhi wa Mazingira, Viwanda na uwekezaji wananchi kiuchumi.
Jumla ya Miradi iliyokaguliwa, kuwekwa mawe ya msingi na kutembelewa jumla ni saba ambapo mitano ilikaguliwa/ kutembelewa na miwili iliwekwa mawe ya msingi. Miradi yote hii ilikuwa na thamani shilingi billion ishirini na saba, million miasaba kumi na nne , sabini na tisa elfu,mia nane kumi na saba na senti ishirini (Tsh. 27,714,079,817.20).
Mzee Mkonge Ali mkuu wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2019 amekagua/kutembelea Mradi uliokamilika wa madarasa matatu pamoja na madawati sitini (60) katika shule ya Msingi Ketumbeine wenye thamani ya Tsh. 53,450,000/= na kuridhika na ujenzi wa Mradi huo. Mradi mwingine ambao uliwekwa jiwe la Msingi na ujenzi wa Bweni la Wasichana wa Tanzania Education and Micro-Business Opportunity (TEMBO Trust) wanye thamni ya Tsh. 207,331,673.20 na kuridhishwa na utekelezaji huo.
Lakini pia Mkongea Ali Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ametembelea na kukagua utekelezaji wa Mradi mkubwa wa Tanki la Maji ambao umefikia 98% kwa thani ya Tsh. 15,793,939,144 na tayali Tsh. 10,195,410,690.78 zimekwisharipwa kwa mkandarasi, ameridhishwa na mwendelezo huo. Hatahivyo ameweka jiwe la Msingi na kuzindua Mradi wa Mali Hai Club na Uhifadhi wa Mazingira katika shule ya Sekondari Longido ambapo ameridhishwa jinsi ambavyo Wilaya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, Mashirika binafsi pamoja na Longido Sekondari kuhakikisha wanatunza Mazingira hasa ndani ya Longido yanayoonekana kuwa na ukame.
Vilevila Ndug. Mkongea Ali alizindua na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kiwanda kikubwa cha usindikaji nyama cha Eliya Food Overseas Ltd ambacho kinalenga kutekeleza Irani ya Chama Cha Mapinduzi ya Serikali ya awamu ya tano kuwa ni Serikali ya Viwanda ambacho ujenzi wake umefikia 70% kinatarajia kukamilika na kuanza uzalishaji Oktoba 2019. Kiwanda hicho hadi kukamilika kwake kinatarajiwa kutumia jumla ya Tsh. 11,600,000,000.00
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM