Watendaji wa kata kutoka katika kata sita zikiwemo kata ya Noondoto, Ilerienito, Gelai Lumbwa, Gelai Merugoi, kamwanga na Elang'hatadapash wamekabidhiwa pikipiki kutoka serikalini ikiwa na lengo la kurahisisha kazi katika utendaji wao kwa jamii.
Akikabidhi pikipiki hizo Mkurugenzi mtandaji wa Halmashauri ya wilaya ya Longido ndugu Stephen A Ulaya leo tarehe 11 /03 /2023 katika viwanja vya Halmashauri, amewataka watendaji hao kuzitumia pikipiki hizo kwa uzuri na umakini wa hali ya juu na kwa madhumuni ya kazi za Serikali na si vinginevyo, pia amewaomba kuzitunza kwa maslahi mapana ya Halmashauri "Ndugu zangu serikali imetoa pesa nyingi sana kwenye miradi ya maendeleo na imeona ni vema pia kutoa pesa kwa ajili ya kununua pikipiki kwa watendaji wa kata, na sisi Longido tumepewa pikipiki sita tafadhali naomba hizi pikipiki ni zetu naomba tuzitunze" Alisema ndugu Stephen Ulaya. Ameongeza kwa kusema "Ni imani yangu pikipiki hizi zitatumika kwa makusudi yaliyokusudiwa sitarajii mtumie tofauti kila mmoja ana wajibu wa kuitunza" Alisema Ulaya
Pia mkurugenzi ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake mama Samia Suluhu Hassan kwa kutoa msaada wa pikipiki kwa watendaji wa kata hizo na ameahidi kuzitunza kwa maslahi mapana ya wananchi wa Halmashauri ya Longido
Pamoja na kuwa serikali imetoa pikipiki sita kwa ajili ya Halmashauri lakini pia Halmashauri imetenga kiasi cha fedha katika bajeti ya mwaka 2023/24 kwa manunuzi ya pikipiki zingine kumi nane kwa kata zilizobakia ikiwa na lengo la kuzifikia kata zote ndani ndani ya halmashauri kwani kitendea kazi hicho ni muhimu na kitarahisisha mawasiliano kulingana na mazingira yetu ya Longido yanayotuzunguka kuwa magumu na kutofikika kwa urahisi "Tumeanza na Kata za mbali kidogo kama tulivyokubaliana katika kikao chetu cha watendaji na baadae tutaleta kwa kata zilizobaki bila upendeleo" Alisema ndugu Stephano Ulaya
Nae Mtandaji wa kata ya Gelai Merugoi ndugu Lesioni Mollel kwa niaba ya watendaji ameishukuru Serikali kwa kuona ipo sababu ya kuwapatia pikipiki hizo kwani zitawasadia hasa katika kuwahudumia wananchi wa kata zao."Tunaishukuru sana serikali hasa ofisi ya Rais Tamisemi kwa kutujali sisi watendaji kwa kata hususani sisi wa kata za mbali kidogo ambapo hapo awali tulikuwa tukipata tabu sana katika kuwahudumia wananchi ndani ya kata zetu sasa kwetu itakuwa rahisi sana kuwafikia wananchi wote kwa kitendea kazi hiki ndani ya kata zetu nami /Nasi tunaahidi kuzitunza na kufanyia kazi zilizokusudiwa na serikali na sio kinyume na hapo.
*Jamhuri ya muungano wa Tanzania kazi iendelee*
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM