Katika kutetea usawa,uwajibikaji,na utawala bora kwa jamii Chama cha wanasheria wanawake Tanzania(TAWLA) kimefanya mkutano wa jukwaa la wanawake na vijana katika halmashauri ya wilaya ya longido mkoani Arusha leo tarehe 15/01/2018.
Mikutano kama hiyo imefanyika katika mikoa mitatu Tanzania nayo ni mkoa wa Arusha,Mwanza na Tanga na kufanyika kwa majimbo matano katika mkoa wa Arusha ikiwa ni Arumeru
( magharibi& mashariki) karatu,monduli na longido. Na lengo kuu ni kuhamasisha wanawake na vijana kushiriki katika nyanja mbalimbali za
uongozi kisiasa katika uchaguzi utakao fanyika 2019/2020.
Wakati akihutubia mkutano huo aliyekuwa mgeni rasmi ndg. Toba Nguvila ameeleza kuwa TAWLA kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo wamekuwa kipaumbele kuhakikisha wanawake na vijana wanatambua haki zao za msingi kwa kushiriki katika nyanja mbalimbali za uongozi kisiasa huku wakimwunga rais mkono kuwa haki na
Usawa katika uongozi ni kazi tu katika utendaji.
Pia kwaupande wao wananchi wameweza kutoa changamoto na maoni yao juu ya changamoto ambazo zinapelekea wanawake na vijana wengi kushindwa kuwania nafasi mbalimbali katika uongozi ambazo ni 1; mfumo dume 2; uchu wa madaraka 3;kukosa ujasiri 4;maswala ya kiuchumi 5;imani potofu 6; mfumo duni kielimu 7 ; mifumo ndani ya vyama vya siasa 8; kujijengea imani kuw kijana nitaifa la kesho hivyo hapaswi kugombea kwa sasa.
Vilevile wametoa maoni yao kuwa ili kutatua matatizo hayo ni vyema kuondokana na fikra potofu,rushwa,chuki na mifumo ndani ya vyama vya siasa.
Hivyo basi wadau hao wa TAWLA ambao ni maafisa wanasheria ndg.Ekaria michael,Neema Ahmed na Silivia Hatbeti wameeleza kuwa pamoja na uhamasishwaji wa wanawake na vijana pia wame anzisha miradi mbalimbali na kwa sasa wakitekeleza mradi wa ( WYPRE) woman & youth Politica Representation Enhanced wenye lengo la kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana watakaowania nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao yaani uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM