Halmashauri ya Wilaya ya Longido Mkuu wa Mkoa wa Arusha Chini usimamizi wa umakini wa hali ya kuridhisha wa Mkurugenzi Mtendaji Ndug. Jumaa Muhina imepewa pongezi kwa uendelezaji mzuri wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo ambao kwa sasa umefikia hatua ya kupaua/ kuwezeka kwa baadhi ya majengo.
Bw. Mrisho Mashaka Gambo mkuu wa Mkoa wa Arusha ametoa pongezi hizo mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea na kukagua mwendelezo wa utekelezaji wa Mradi huo unaotekelezwa ndani ya Wilaya ya Longido na kujionea jinsi namna ujenzi unavyoenda kwa kasi.
Bw. Gambo amesema kuwa Mkoa wa Arusha umepata fursa ya kipekee ya kujengewa vituo vya Afya na Serikali ya awamu ya tano katika maeneo mbalimbali na kuwataka Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi pamoja na wahusika wa utekelezaji wa Mradi huo mkubwa Longido kufanya kazi usiku na mchana ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Mgufuli kwa kauli mbiu ya ‘HAPA KAZI TU!’.
Aidha Gambo amesema kuwa Mradi wa utekelezaji ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ulitarajiwa kumalizika mwezi Mei 2019 lakini kutokana na ukubwa wa Mradi pomoja na vifaa kutoka mbali huku vikitumika kona nyingi za Tanzania ambazo Hospitali/Vituo vya Afya vinajengwa upelekea Mradi huo kuongezewa muda. Vilevile Bw. Gambo amewasihi kuhakikisha kufika mwezi Juni 30, 2019 Mradi huo uwe umekamilika.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mhe. Frank James Mwaisumbe amesema kuwa utekelezaji wa Mradi huo mkubwa ndani ya Longido pindi utakapokamilika utawaondolea hadha wakazi wa Longido ya kusafili umbali mrefu kwenda Arusha ama KCMC kutafuta matibabu, Wasafili wanaotoka ama kwenda nchi jirani Kenya kwa maana Mradi upo karibu na barabara kwahiyo utatoa huduma kwa haraka, magonjwa ya akina mama na watoto yatatatuliwa, upasuaji pamona na huduma nyingine za kiafya ambazo zimekuwa zikiwasumbua wanalongido zitapatiwa majibu.
Hata hivyo Mhe. Mwaisumbe amefafanua kuwa Mradi huo unajumla ya majengo saba (7) yanayo jumuisha Wodi ya wazazi, jingo la upasuaji, Wodi ya kulaza wagonjwa, Wodi ya akina mama na watoto, Chumba cha dharura na maeneo mengine kwa ajili ya kutoa huduma za kiafya.
Amehitimisha kwa kusema kuwa Wilaya kwa kushirikiana na Mkurugenzi wakuu wa Idara, Engineer kutoka Arusha wamekwisha ridhia toka awali kufanya kazi usiku na mchana ili kumaliza kwa wakati.
Naye mkurugenzi Jumaa Mhina amesema ujenzi umefika hapa mahala pazuri kwa ushirikiano mkubwa wa Serikali pamoja na Wanalongido kwa ujumla kwa kujitoa usiku na mchana kuiunga mkono serikali ya Tanzania.
Pia ameendelea kusema kuwa Serikali imetupa kipaumbele cha kutujengea Hospitali kubwa Ya Wilaya hivyo na wao kama Halmashauri wanajibbika kwa kutekeleza Mradi huo kwa kiwango stahiki na kwa muda muafaka.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM