Mkuu wa wilaya ya Kinondoni , mheshimiwa Daniel G.Chongolo amewaaga rasmi watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Longido na kuwakabidhi kwa Mkuu wa wilaya mpya ya Longido Mheshimiwa Frank Mwaisumbe hapo jana,
Akiongea wakati wa makabidhiano hayo mheshimiwa Chongolo amesema anawaamini watumishi wa longido hana shaka nao ni wachapakazi na wamekuwa msaada mkubwa kwake kwani bila wao asingeweza kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Hata hivyo amewataka watumishi wa halmashauri ya Longido kumpa ushirikiano mkubwa Mheshimiwa Mwaisumbe kama ule aliokuwa anapewa yeye katika kipindi chote alichofanya kazi Wilaya ya Longido.
Mheshimiwa Chongolo amekiri, kuridhishwa na uwezo wa watumishi wa halmashauri ya Longido na hakusita kuwapongeza watumishi hao mbele ya mkuu huyo mpya wa wilaya ya Longido
" Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Longido,Watumishi hawa wana uwezo mkubwa wa kufanya kazi ukiacha kasoro ndogondogo sina shaka nao hata kidogo na uwezo wao wa kufanyakazi kwa weledi amesema Mheshimiwa Chongolo.
Ameongeza kuwa, kwa kipindi alichofanyakazi wilaya ya Longido, amekiri kuona utendaji uliotukuka wa watumishi wa halmashauri ya Longido wa kujikita zaidi kwenye kazi za kuhudumia wananchi.
Nao watumishi wa halmashauri ya Longido, wamempongeza mkuu huyo wa wilaya ya Kinondoni na kuthibitisha kuwa wamefanikiwa, kujifunza mambo mengi kutokana na weledi wa kufanya kazi na kujitoa kwa Mheshimiwa chongolo. amekua akituonyesha mwelekeo ametuonyesha dira hakika tutamkumbuka sana Mheshimiwa Chongolo wamesema watumishi hao.
Wamesema kuwa uchapakazi na kujitoa kwa Mheshimiwa Chongolo, , ni funzo kubwa kwa watumishi wa halmashauri ya Longido na kuahidi kuendeleza katika kuwatumikia wananchi wa Longido.
Naye Afisa Manunuzi , halmashauri ya Longido, Cleophas Tenganamba amesema kuwa amejifunza, kujishusha na uchapakazi na urafiki aliojenga bila kujali hadhi yake pamoja na kutumia muda zaidi katika kufuatilia jambo.
" Mheshimiwa Chongolo ni kiongozi anayefatilia jambo na mnatekeleza wote kama sehemu ya mtumishi ni wa tofauti sana na viongozi wengine licha ya kuwa na cheo kikubwa, lakini ni bado ni anayejishusha, mwenye kusikiliza na kufanyia kazi jambo kwa muda kabla ya kufanya maamuzi, kifupi ni kiongozi mchapakazi" na namuombea sana kwa Mungu ambariki amesema Afisa Manunuzi huyo.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa Frank Mwaisumbe akiongea wakati wa makabidhiano hayo amesema kikubwa anaomba ushirikiano na nguvu zaidi iongezwe kwenye ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuzuia mianya yote ya upotevu wa mapato.
"Nitaifanya longido iwe kitovu cha utalii, utalii wa picha,utalii wa ndege n.k ili kuongeza mapato katika wilaya yetu" amesema mheshimiwa mwaisumbe.
Pia amewataka watumishi kila mmoja asimame katika nafasi yake na kufanya kazi kwa weredi ili kuleta ufanisi na ubora na amehaidi kufuatilia na kutetea maslahi ya watumishi wote bila upendeleo wowote.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM