Timu ya wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nkinga mkoani Tanga leo tarehe 30/11/2020 wametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Longido kujifunza jinsi Halmashauri ilivyoweza kukusanya mapato ya Mpakani kupitia ushuru wa mazao yanayovuka mpaka, Ushuru wa kuvuka mpaka wa Malori(Boarder closing fee) Ushuru wa Mifugo na ushuru wa vyanzo vingine.
Timu hiyo imeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ndugu Rashidi Gembe aliyeambatana na Afisa Biashara Bi Christina Kileo ,Afisa Mipango ndugu John na Mweka hazina ndugu Geofrey Julius.
Akiongea na ugeni huo katika eneo la mnada eworendeke Dkt Jumaa Mhina Mkurugenzi Mtendaji alisema tumewez kupandisha amapato ya serikali kuu kupitia mnada huu wa mifugo wa eworendeke uliojengwa kwa ufadhili wa Programu ya MIVARF ambapo wizara ya Mifugo wamekusanya wastani wa bilioni 300 na Halmashauri tumekusanya takribani bilioni 1.2 kupitia mnada huu toka umeazishwa.
Pia timu hiyo imeweza kutembelea kiwanda cha kuchakata nyama kinachojengwa na mwekezaji Elia food overseas,wakiwa kiwandani hapo Dkt Mhina alisema kiwanda hiki kimeshaanza kazi ambapo Halmashauri inategemea kupata mapato kutokana na kodi ya huduma na ushuru wa ukaguzi wa nyama(inspection fees) na tutaweza kutekeleza Miradi yetu ya Maendeleo lakini pia serikali kuu itapata mapato alisema Dkt Mhina.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nkinga, Ndg Rashid Mgembe amemshukuru Dkt Mhina kwa ziara yao yenye mafanikio makubwa na kusema hakika ni Wilaya ya Mpakani inayofaa kuigwa na Halmashauri za mpakani.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM