• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Miundombinu, Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mjjini
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Utawala na Usimamizi wa Rasimamli Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Utalii
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Leseni
    • Huduma za Utalii
    • Huduma za Mapato
    • Huduma zetu Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati ya Maadili ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Barua pepe za Idara na Vitengo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Kituo cha habari
      • Maktaba ya Picha
      • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
  • Vivutio
    • Mbuga
    • Ziwa

Serikali yahuisha fedha za mradi wa TASAF kwa walengwa wa kaya maskini.

Posted on: May 24th, 2018

Halmashauri ya Longido  leo tarehe 24/05/2018  imeanza zoezi la kuhuisha fedha za Mpango wa Kunusuru kaya Masikini zinazotolewa na serikali kupitia mradi wa TASAF awamu ya III kwa wanufaika wa Mpango huo.

Afisa mzimamizi wa zoezi hilo kutoka halmashauri Jimmy akizungumza wakati wa zoezi  hilo amesema  tumejipanga kutumia muda mfupi kabla ya kugawa fedha kwa lengo la kuwakumbusha wanufaika wa mpango kutumia fedha hizo kutokana na masharti ya TASAF.

Jimy amefafanua kuwa kuna baadhi ya wanufaika wanashindwa kutekeleza masharti ya matumizi ya fedha hizo ikiwemo kuwahudumia watoto wanaosoma, kuwapeleka watoto kliniki pamoja na kuhudumia familia na badala yake wanatumia fedha hizo kwenye ulevi.

"Inatulazimu kuwakumbusha wasimamizi hawa wa kaya kutumia fedha hizo kutunza familia kwa kuwa imeonekana baadhi yao wakipata hela wanaishia kwenye pombe na kusababisha familia kuendelea kuteseka" amesema Jimy

Jimy ameongeza kuwa mafunzo tutakayoendelea kuyatoa pamoja na ufuatiliaji wa karibu wa wanufaika hao yatasaidia kutatua changamoto hiyo kuliko kukaa kimya kuwaacha bila kuwakumbusha.

Hata hivyo wasimamizi wa kaya hizo waliofika kupokea ruzuku hizo wanajivunia kuwa mradi huu umefanya afya zao kuboreka na watoto wao kupata elimu ya uhakika.

Wameongeza kuwa kwa sasa makali  ya gharama za matibabu pia imepungua kwani wana Bima za afya zinazowasaidia kupata matibabu na wategemezi wao bila shida yoyote.

Naye mratibu wa TASAF halmashauri ya Longido Lobulu S.Saruni amesema kuwa kwa sasa wanalipa awamu ya tatu tangu mradi huo kuanza na awamu hii wamelipa jumla ya shilingi milioni 197.77 kwa kaya 5,641 kwenye vijiji  27 ndani ya halmashauri ya Longido.

Lobulu amesema kuwa licha ya kuwa fedha hizo zinawasaidi wananchi hao lakini bado kuna changamoto ya baadhi ya wanakaya kushindwa kutimiza masharti jambo ambalo linasababisha mwana kaya kukatwa kiasi cha fedha.

Hata hivyo Lobulu amesema kuwa kupitia maafisa wa halmashauri wanaokwenda kusimamia zoezi la ulipaji wa fedha kuhakikisha wanatoa mafunzo ya kuwakumbusha wanufaika hao kutumia fedha hizo kulingana na masharti ya TASAF.

Aidha amewataka wananchi wote wanaonufaika na Mpango kutumia fedha hizo vizuri pamoja na kutunza vitambulisho vyao vya TASAF na kuepuka kutuma mtu wa kumchukulia fedha jambo ambalo haliruhusiwi na linasababisha fedha kurudishwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA June 13, 2025
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WA UMMA April 12, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA May 15, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA June 25, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • View All

Video

MKUU WA WILAYA YA LONGIDO AUNGANA NA RC KIHONGOSI KWENYE JOGGING YA TANZANIA SAMIA CONNECT
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.