"Nashindwa niseme kwaheri World vision au niseme nini? Ila tuache hivyo hivyo hewani , ni imani yangu kubwa mtarudi tena kuwasaidia watu wa Ketumbeine "Ni maneno yake Mheshimiwa Marco Henry Ng'umbi mkuu wa wilaya ya Longido
leo tarehe 30/08/2023 kwenye viwanja vya Ketumbeine alipokuwa akiliaga rasmi Shirika la World vision lilokuwa limejikita kwenye miradi mbali mbali ya Maendeleo kwa takribani miaka kumi na mitano kwa wananchi wa Kata ya Ketumbeine.
Shirika la World vision ambalo linafadhiliwa na nchi ya Canada lilianza shughuli zake katika kata ya Ketumbeine kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Longido mnamo mwaka 2009 Amabapo lilianza rasmi kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwenye Tarafa hiyo yenye kata takribani 6 zenye shule na vituo vya Afya mbapo leo limekamilisha muda wake Wilayani humo
Shirika hili limekuwa likitoa misaada mbali mbali kwa jamii hiyo ya Ketumbeine katika nyanja tofauti kama chakula kwenye shule za msingi likiwa na lengo la kuongeza na kuhamasisha watoto waweze kusoma bila usumbufu wowote na kutengeneza mazingira bora ya kujifunza,Sambamba na hilo Shirika limejenga bweni kwa ajili ya watoto wa kiume ili kuwasaidia watoto wanaotoka kwenye jamii ya wafugaji hasa wanaotoka mbali na kutembea kwa umbali mrefu World vision pia imetoa msaada kwenye idara ya Afya kwani limejenga jengo la mama na mtoto kwenye Kituo cha Afya Ketumbeine, jengo hilo limeanza kutumika kwa kuzalisha na kutoa huduma ya Afya ya mama na mtoto, Sambamba na hilo pia Shirika limetoa msaada wa kiuchumi kwa wakazi wa kata ya Ketumbeine yaani vijiji vya Noondoto, Gelai Lumbwa, Gelai Merugoi Ilerienito Elang'hatadapash, pamoja na Ketumbeine yenyewe kwa kuwapatia wananchi hao mbuzi, kondoo na Ng'ombe ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Akilishukuru shirika hilo Mh Ng'umbi amewaasa wananchi wa kata hiyo kuyatii na Kuyaendeleza yote mazuri yaliyofanywa na Shirika hilo ikiwa sambamba na kuahidi kusimamia vyema miradi iliyoachwa na Shirika hilo.
Naye mkurugenzi wa shirika la World vision amewashukuru Wananchi wa Tarafa hiyo kwa utulivu na ushirikiano wao waliouonesha kwa Shirika kipindi chote cha utekelezaji wa Miradi hiyo ya Maendeleo katika kata hiyo "Wanajamii wa Ketumbeine bado mko kwenye Mioyo ya World vision hivyo haitakuwa mwisho wa sisi kushirikiana nanyi katika mambo mbali mbali sisi tupo tutao msaada na ushauri pale mtakapo hitaji ushauri i wetu Asanteni sana. Alisema Mkurugenzi huyo
Akuzungumza Kwa niaba ya wananchi wa Ketumbeine mama Loserian Mollel amelishukuru shirika la World vision pamoja na Serikali kwa kuichagua Ketumbeine na kuleta miradi yenye Tija na manufaa kwa wananchi "Kweli kabisa tunashukuru sana mana sasa nimeweza miliki Ng'ombe wa Maziwa wananisaidia kupeleka watoto shule kuwanunulia mavazi wakati hapo mwanzo sikuweza kabisa" Alisema mama huyo mkazi wa Ketumbeine.
Shirika limefikia tamati katika kazi zake leo na imekabidhi miradi yote iliyotekelezwa kwa serikali ya Halmshauri ya Wilaya ya Longido ikiwa ni miradi ya Elimu, Afya Maji pamoja na miradi ya Kiuchumi.
*Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kazi iendelee*
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM