NA ABRAHAM NTAMBARA
Katika kuunga mkono Kampeni ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia, Shule ya Sekondari Natron Flamingo's iliyopo Kijiji cha Meirugoi, Kata ya Gelai Meirugoi, wilayani humo, mkoani Arusha imefunga mfumo wa gesi na kuanza kupikia chakula cha walimu na wanafunzi shuleni hapo.
Kufungwa kwa mfumo huo ni utekelezaji wa maagizo ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Longido aliyoyatoa mwaka jana shuleni hapo ya kutaka kuanza kutumika kwa nishati safi ya kupikia badala ya kuendelea na mazoea ya kutumia kuni lengo likiwa ni kuunga mkono kampeni ya Serikali ya kuhamasisha matumiza ya nishati safi ya kupikia nchin.
Akizungumza Oktoba 13, 2025 baada ya kutembelea na kujionea mfumo huo na namna unavyofanya kazi, Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Longido Mwl. Gilbert Sombe aliupongeza uongozi wa shule hiyo chini ya Mwalimu Mkuu Hassan Hassan kwa kutekeleza maagizo yake kwa haraka na kwa wakati.
Hata hivyo Mwl. Sombe alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa Shule nyingine za Sekondari wilayani humo kuhakikisha zinaiga mfano wa Shule ya Natron Flamingo's na kufunga mfumo huo na kuachana na matumizi ya kuni ambayo yanaharibu mazingiri na nihatari pia kwa afya.
"Nipende kuupongeza uongozi wa shule chini ya Mwalimu Mkuu kwa kufunga mfumo huu na nitoe wito kwa Walimu Wakuu wa Shule zingine kuiga mfano huu, wafunge mfumu huu wa gesi kwani ni mzuri na rahisi badala ya kuendelea kutumia kuni," alisema Mwl. Sombe.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Hassan Hassan alisema mfumo huo ulianza kutumika tangu Septemba 5, 2025 na kwamba una majiko tisa (9) ambapo kati ya hayo majiko nane (8) ni kwa ajili ya kupikia chakula cha Wanafunzi huku jiko Moja (1) likiwa ni kwa ajili ya kupikia chakula cha walimu.
Alisema kuwa matumizi ya nishati ya gesi kwa kupikia ni rahisi na chakula huiva vizuri tena kwa muda mfupi na kuifanya gesi kutotumika sana kwani tangu waanze kuitumia hadi sasa wemeshatumia nusu tu ya gesi hiyo, ikilinganishwa na kipindi ambacho walikuwa wakipika kuni.
Havyo alisisitiza kuwa matumizi ya nishati hiyo ni salama kwa mazingira na afya kwa binadamu, na kwamba wamefanya hivyo ikiwa ni utekelezaji wa melekezo ya Serikali ya kutumia nishati safi ya kupikia.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.