Katika kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli Halmashauri ya Wilaya ya Longido kupitia Ofisi ya Mpango (TASAF) imeendeleza utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo pamoja na Miradi ya kutoa ajira kwa muda mfupi kwa Kaya maskini ndani ya Wilaya hiyo.
Akitoa ufafanuzi Mratibu wa Mpango (TASAF) wa Wilaya Ndg. Lobulu Saruni Ofisini kwake Juni mosi 2019 amesema kuwa TASAF Wilaya ya Longido imefikia hatua nzuri kimaendeleo katika kuhakikisha inatoa huduma za maendeleo kwenye jamii.
Aidha Lobulu amedai kuwa Miradi yote ya Maendeleo inayotekelezwa chini ya usimamizi wa TASAF katika Wilaya ya Longido, baadhi imekwisha kukamilika kwa asilimia miamoja (100%) na mengine ikiwa katika utekelezaji kwa asilimia 65% na kuendelea.
Hata hivyo ametaja Miradi ya Maendeleo inayetekelezwa na TASAF kuwa ni utekelezaji wa Miundombinu ya Elimu kwa ujenzi wa Nyumaba za Walimu two in one katika Shule ya Msingi Ilchang’itsapukin Mradi abao ulianza kujengwa mwezi Februali 2019 na wenye thamani ya fedha za kitanzania Tsh. 76,112,825.75 na unatarajiwa kumalizika Mwishoni mwa mwezi juni 2019.
Pia TASAF Longido ipo katika utekelezaji wa ujeni wa Vyumba vya Madarasa 2, Ofisi ya Walimu na Vyoo matundu 6 katika Shule ya Ilchang’isapukin wenye thamani ya Tsh. 72,283,501.71 ambao upo katika hatua za mwisho na pia Lobulu amesema upo Mradi wa ujenzi wa Uzio wa Shule ya Msingi Ilchang’itsapukin wenye thamani ya Tsh. 71,817,248.37 na utekelezaji tayari Ukuta (Uzio) umekwishaanza kujengwa.
Mradi wa utekelezaji wa ujenzi wa Bweni la Wanafunzi Shule ya Sekondari Endaimet wa Tsh. 71,677,101.26 na upo katika hatua za umaliziaji, ujenzi wa Zahanati Kijiji cha Olchoroonyokie ambao utagharimu Tsh. Milion Miamoja na mbili (102,000,000) na Fedha ambazo zishapelekwa ni Milion Sabini na Moja (71,000,000) wakati huo taratibu za kupeleka Fedha za umaliziaji zimekwishaanza.
Vilevila Lobulu ametolea ufafanuzi wa juu ya Miradi ya kuta ajira kwa muda mfupi kwa Walengwa ambao ni Kaya Maskini yaani Public Work Programme (PWP) kuwa ni ukarabati wa Barabara ya Jamii Km 7 kijiji cha Alaililai ambao utagharimu Tsh. 731,834,084.48, Barabara ya Jamii Km 6.5 Kijiji cha Sakane wa Tsh. 74,401,078.60, Barabara ya Jamii Km 10 Kijiji cha Olmolog Tsh. 73,878068.81 huku akisema kuwa utekelezaji wa Barabara zote umefikia asilimia 65%.
Lobulu amebainisha Miradi iliyokwisha wafikia Walengwa kwa asilimia 100% kuwa ni Ufugaji wa kuku wa Kienyeji katika Vijiji vya Mundarara , Mairouwa na Irkaswa ambapo kila kijiji kilikuwa na Walengwa 75 na vilipata idadi sawa ya Kuku 825 kwa huku kila kijiji kikiwa na thamani ya Tsh. 22,947,808.45.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM