Timu hiyo ilifanya kikao mapema leo,na imetaka kujua namna malalamiko ya Watumishi wa Halmashauri yanavyoshughulikiwa,hatua zinazopitiwa na kuhakikisha malalamiko ya Watumishi yanatatuliwa kwa wakati,uwazi na haraka.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Wakuu wa Idara ,na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya.
Aidha Afisa Utumishi Bw. Steven Mbombe amesema “njia wanazotumia Watumishi kuwasilisha malalamiko yao ni Barua,Majalada na Sanduku la maoni.
Hata hivyo Mbombe aliongeza kwa kusema kuwa Mtumishi anayeshughulikia malalamiko hayo yupo masomoni.”
Timu hiyo ya Wataalamu wamewashauri Watumishi kuwa wawepo wataalamu watatu wa kushughulikia malalamiko ya watumishi ili kazi hiyo ifanyike muda wote saa za kazi.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM