Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Kifungu cha 13(3) imetoa taarifa ya kufanyika kwa Uchaguzi Mdogo wa Udiwani tarehe 12 Agosti 2018 kwenye Kata ya Kamwanga, Elang’atadapash na Olmolog. Nafasi wazi zilitokana na Madiwani wa Kata hizo Ndg Jacob Silas Mollel (Elang’atadapash – CHADEMA), Ndg Elias Mepukori Mbao (Kamwanga – CHADEMA) na Ndg Diyoo Lomayani Laizer (Olmolog – CHADEMA) kujiuzulu nafasi zao Januari Mwaka huu.
Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na Tume, zoezi la kutoa Fomu za Uteuzi litafanyika kati ya tarehe 08 hadi 14/07/2018, Uteuzi wa Wagombea ni tarehe 14/07/2018, kampeni za Uchaguzi ni tarehe 15 Julai hadi 11 Agosti na Upigaji Kura utafanyika tarehe 12/08/2018
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Longido Ndg Jumaa Mhina amewahakikishia Wananchi wa Kata hizo kuwa Uchaguzi utakuwa wa amani, huru na haki na akatoa rai kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kutimiza wajibu wao wa kidemokrasia kwa kuwachagua Viongozi wanaowataka ili kuwawakilisha kwenye Baraza la Madiwani. Aidha alisema Ofisi yake itatoa ushirikiano unaohitajika ili kufanikisha zoezi hilo na akawataka wasisite kuwasiliana na Afisa Uchaguzi na Utawala Bora wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Ndg Constantine Mnemele kupitia namba 0786 784 265.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM