Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo ameiomba Wizara ya Kilimo na Mifugo kuzitafutia ufumbuzi changamoto walizozitoa wafanyabiashara wa Soko la kuuza na kununua Mifugo la Eworendeke lililopo Namanga Wilayani Longido mkoani Arusha.
Maombi hayo ameyatoa leo jioni juni 20, 2019 wakati akilasimisha/kufungua Soko hilo ambalo linalenga kutatua changamoto za wafanyabiashara wa Mifugo, kukuza uchumi pamoja na kuitangaza nchi kwa kutoa huduma ya mifugo na nyama kila siku.
Mhe. Gambo ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kuwa malengo ya kulasimisha soko hilo ni kuondoa utoroshwaji wa mifugo bila kufuata utaratibu, Kupunguza kodi zisizo za lazma kwani wafugaji wanafanya kazi kubwa ya kuchunga ng’ombe na kuwatunza, kutengwa kwa mapato ya serikali na haki ya mfugaji ili maji barabara,elimu bure na miundombinu nyingne ziweze kujengwa.
Aidha amesema kuwa baada ya kufungua soko hilo mkoa utaimarisha ulinzi wa mipaka mara dufu na kuchunguza kwa umakini kule wafanyabiashara wanakouza ng’ombe kama wameuzwa kwa njia halali ili kuhakikisha muuzaji na mnunuzi wote wanapata haki zao na pale itakapobainika mifugo inatoroshwa wahusika watawajibishwa.
Vilevile amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Longido kuandaa kikao cha kuwakutanisha wafanyabiashara wa pande zote mbili yaani Tanzania na Kenya ili kuondoa utofauti na kama akishindwa amtaarifu mkuu wa Mkoa na mkuu wa mkoa akishindwa bazi Wizara itapatiwa taarifa kikubwa mpaka mwafaka upatikane.
Hata hivyo amezungumza kwa ukali kuwa Tanzania itaendelea kuwa ujinga mpa lini kwa kuuza mbuzi Kenya na Kenya kusifika kwa umaarufu wa kufuga kuliko Tanzania “ tutaendelea kuwa wajinga mpa lini tunawauzia mifugo yetu kwa gharama nafuu na mkifika huko mnatamba kuwa mifugo hiyo ni ya kwenu na kupata umaarufu nje ya nchi nasikia huko India tutashindwana kama ni hivyo” Mhe. Gambo
Kwa upande wake Katibu mkuu Wizara ya kilimo na uvuvi Mhe.Elisante Ole Gabriel aliye mwakilisha Waziri wa Kilimo na Mifugo amesema kuwa swala la ufunguzi wa soko hilo la kimataifa litaleta neema katika nchi kwani toka 2001 mapendekezo yalikuwepo na mwaka agosti 31, 2019 mradi huo ulipitishwa kuwa mnada wa mpakani.
Mhe. Ole amesema kuwa jitihada zilizofanywa na Ofisi ya Waziri mkuu, Mkoa, Wilaya pamoja na wadau wengine vimekuwa chachu kubwa katika ujenzi mpaka kufikia hatua za ufunguzi. Pia amesema kuwa Waziri amemwagiza kuwa wafanyabiashara wasidhubutu kutorosha mifugo.
Ameendelea kusema kuwa Wizara inategemea wananchi wafuge kwa tija, wasijivunie idadi ya ng’ombe bali wajivunie uzito wa ng’ome, na mnada usiwe patio la mifugo bali wapime ng’ombe wauze kwa kilo.
Mhe. Frank Mwaisumbe Mkuu wa Wilaya Longido amesema kuwa ataandaa kikao cha wafanyabiashara wa mifugo na mmiliki wa kiwanda kikubwa kinachojengwa ili kujua nini atahitaji kwao na wao wamweleze nini wanahitaji kwake. Vilevile ametaja siku za juma tatu na juma nne ni kuuza mifugo tu, juma tano licha ya kuuza mifugo lakini kutakuwepo mnada yaani kuchoma nyama, kuchinja n.k, alihamisi – jumamosi ni kuuza mifugo tu na juma pili kutakuwepo na michezo mbalimbali kwaajili ya kutangaza utalii na huduma zinazopatikana sokoni hapo.
Ufunguzi huo umehudhuriwa Mkuu wa Wilaya wa Monduli Mhe. Idda Kimanta, mwakilishi wa DC upande wa kenya Steven Komara ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido Mhe. Sambore Molloimet,Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Longido Ndg. Jumaa Mhina, wafanyabiashara, wakuu wa usalama pamoja na wananchi
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM