USAINISHAJI WA MIKATABA YA LISHE.
Leo tarehe 22.08.2019 katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa wilaya Longido, watendaji wa vijiji vyote wilayani Longido wamesaini mikataba ya lishe mbele ya mkuu wa wilaya Mhe. Frank James Mwaisumbe na afisa afya mkoa wa Arusha Vones Z uiso pamoja na afisa lishe wilaya Adelini Kahija, Zoezi hili litasaidia kutokomeza udumavu na kuinua kiwango cha hali ya lishe wilayani Longido. Watendaji pamoja na wakuu wa idara za halmashauri walipewa elimu ya lishe hivyo watendaji wote wametakiwa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa lishe kwa watu wote.
Watendaji wote wamesaini mikataba hiyo na kuahidi ushirikiano wa kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na udumavu kabisa katika wilaya yetu ya Longido.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM