Halmashauri ya wilaya ya longido Leo tarehe 31/10/2017 imetoa mkopo usio na riba wa fedha za kitanzania sh.42,630,000/- kwa vikundi kumi na moja vya kina mama, vijana na walemavu
Kaimu Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Wilaya Nd. Raymond Mushi wakati wa sherehe za makabidhiano hayo amesema vikundi hivyo ni vya Wanawake,Vijana na Walemavu ambavyo vinajishughulisha na ufugaji, ushonaji shanga na urembo wa kimasai,vikoba na biashara ndogondo.
Mushi amevitaja vikundi hivyo ni Tenebo,Nasaruni parmanja,,Osotwa,Yeyowomen group,Tobiko,Naramatisho,Mshikamano,Amani na Upendo,Upendo groupA2017,Nasaro na Nyangulo armanie.
Pia Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Nd. Jumaa Mhina wakati wa makabidhiano hayo amesema pesa hizo zinazotolewa za mikopo ni za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido na mkopo unatolewa bila riba yoyote kwa vikundi vyote ikiwa ni kutekeleza agizo la Mh Rais wa awamu ya tano Mh.John Pombe Magufuli la kutoa asilimia 10% ya mapato ya ndani kwa wanawake asilimia 4%,vijana asilimia 4%, walemavu asilimia 2% na mkopo huo usio na riba kwa robo hii ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019 umetolewa kwa asilimia 100% .
Akikabidhi mikopo hiyo mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Longido ndg.Frank Mwaisumbe ,amewaasa wanavikundi kuwa pesa zinazotolewa Leo ni kwa ajili ya kukuza uchumi na kuongeza kipato cha wanavikundi na si kwa matumizi mengine lakini pia amewasisitiza kurudisha mikopo hiyo ili isaidie na wahitaji wengine.
Nae Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha Ndg. Loth Sanare ameupongeza uongozi wa wilaya kwa kazi nzuri ya kufanya hitaji la kisheria la kutoa asilimia mia moja ya mkopo kwa vikundi mbalimbali lakini pia kuwa mstari wa mbele katika kushughulikia shida za wananchi kama anavyotutaka Mh.Rais wetu wa awamu ya tano kuwa tushughulike na shida za wananchi.
Mwenyekiti Sanare pia ameviasa vikundi vyote kurudisha mikopo hiyo kwa wakati pindi muda utakapofika ili vikundi vingine vipate mikopo hiyo.
Vile vile vikundi vilivyopata mikopo wametoa shukrani zao za dhati kwa Halmashauri ya Longido na kuahidi kutumia mikopo hiyo kama ilivyokusudiwa.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM