Na Happiness Nselu
Longido, Arusha - Viongozi wapya wa serikali za mitaa katika Wilaya ya Longido wameapishwa rasmi leo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, watendaji wa halmashauri, na wananchi waliokuja kushuhudia tukio hilo muhimu.
Hakimu mfawidhi wa Wilaya ya Longido Mh.Eliarusia R.Nassary aliwaongoza viongozi hao katika kiapo cha uadilifu na uwajibikaji. Akizungumza baada ya kuwaapisha,Bw. Joseph Logolie aliwahimiza viongozi hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa weledi, uwazi, na kushirikiana na wananchi katika kusukuma mbele maendeleo ya jamii zao.
“Uongozi ni dhamana, na jukumu lenu kubwa ni kuhakikisha mnatoa huduma bora kwa wananchi wenu. Msikilize matatizo yao, tafuteni suluhisho kwa kushirikiana, na hakikisheni mnazingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma,” alisisitiza Bw Logolie.
Viongozi walioapishwa ni pamoja na wenyeviti wa vijiji, wenyeviti wa vitongoji, na wajumbe wa halmashauri kundi la wanawake pamoja na wajumbe kundi mchanganyiko mbalimbali Pia walikabidhiwa nyaraka muhimu zinazowaongoza kutekeleza majukumu yao, ikiwa ni pamoja na mwongozo wa usimamizi wa miradi ya maendeleo na utawala bora.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake, Mwenyekiti mpya wa Kijiji cha Orkojoolengush Bw.Lekshon Kaika Mollel aliahidi kuwajibika kwa moyo wa dhati na kuhakikisha wanashirikiana na wananchi kuboresha maisha ya jamii.
Kufuatia kuapishwa kwao, viongozi hawa wanatarajiwa kuanza mara moja kusimamia shughuli za maendeleo katika maeneo yao, kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya kuhakikisha Longido inaendelea kupiga hatua katika nyanja za kijamii na kiuchumi.
“Kwa pamoja tutaweza, na Longido itaendelea kuwa mfano wa kuigwa katika uongozi na maendeleo,” alihitimisha Bw. Joseph
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM