Viongozi wa Umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido wamekumbushwa kuzingatia maadili ya viongozi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kuondoa mgongano wa Maslahi na kuleta ufanisi wa kazi Serikalini leo Mei 29, 2019.
Akitoa mafuzo kwa Watumishi wa Umma Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini-Arusha Anna Anthony Mbasha yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri (Nyerere) amefafanua kuwa viongozi wa Umma wamekuwa wakisahau majikumu stahiki pindi wanapotekeleza shughuli za kiserikali.
Mbasha amesema kuwa Mgongano wa Maslahi kwa Watumishi wa Umma unakuja pale Mtumishi anapotumia Mdaraka kujinufaisha mwenyewe, kutumia muda wa Ofisi kufanya mambo yake, kutumia vifaa vya Ofis (Simu, Kompyuta n.k.) kutekeleza majukumu banafsi na mengine mengi ambayo yanalenga kunufaisha upande mmoja.
Hata hivyi Mbasha amesisitiza swala la kuwa na Kamati ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Wilaya, inayofanya kazi sambamba na Ofisi ya Mkurugenzi kwa kuhakikisha Watumishi hawaendi kinyume na matakwa ya Serikali.
Mwisho Mbasha ameendeelea kesema kuwa Viongozi wa Umma hawaruhusiwi kutoa ama kupokea zawadi yeyote kwa mto yeyote, kujirimbikizia Mali, kutumia Vyeo kuwanyanyasa wengine kwa maslahi ya aina yao wenyewe.
Awali akikaribisha Mafunzo hayo ambayo kimsing amesema yalifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjoaro Anna Mgwila kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Longido Katibu Tawala Toba Nguvila amesema kuwa Miradi inayotekelezwa na serikali inaweza kukwama kama Viongozi wa Umma watakosa uhadilifu.
Aidha Mguvila ameeleza kuwa Viongozi wamekuwa na Tabia ya kutaka kusimamia wenyewe Miradi inakuwa inatekelezwa na Serikali jambo ambalo upelekea Watumishi wenzao kushindwa kuwawajibisha pale unapokuwa na makosa ya chini ya Kiwango ile hali ya kuwa wote watumishi na wanatokea sehemu moja .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Mhe. Jumaa Mhina akifungua Mafunzo hayo amewataka Watumishi kuzingatia taratibu za kiutumishi, Maadili na Uadilifu wakati wote. “Viongozi wote wa Umma na wanasiasa tunatakiwa kuwajibika kikamilifu wakati wote tunapokuwa katika utekelezaji wa shughuli za serikali” Mhe. Mhina
Vilevila Mhe. Mhina amesema kuwa Selikali inayo Mihimili mitatu Mahakama, Bunge na Utawala ambazo zinatakiwa kuwajibika kutekeleza majikumu ya kiserikali ipasavyo na ndio maana katika mafunzo hayo viongozi wa haina hiyo wote wamejumuhishwa kuleta ufanisi. “Madiwani, Wakuu wa Idala zote, Maafisa wa polisi pamoja mafunzo haya yanawahusu kwa kiasi kikubwa ili kujikumbusha uadilifu, uwajibikaji katika kipindi chote cha uongozi” Mhe. Mhina.
KAIMU MWENYEKITI
Watu wanahitaji sana elimu yam AADILI KWA WAtumishi wa umma kwahiyo iendelee kuja hasa kwetu sisi viongozi ili tuendelee kutekeleza katika kutii uadilifu kwa wananchi.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM