Halmashauri ya Wilaya ya Longido chini ya Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Jumaa Mhina pamoja na Wilaya kwa ujumla chini ya Mhe. Frank James Mwaisumbe imejidhatiti kuzidi kujiweka karibu na Wafanyabiashara wote wa wilaya hiyo huku ikionesha kuwajali na kuwathamini kama ilivyo kwa muhudumu na glas.
Mkuu wa Wilaya Longido Mhe. Frank James Mwaisumbe amefanya kikao na wafanyabiashara wote wa wilaya hiyo wakuu wa Idara mbalimbali zinazohusika na biashara ndani ya Longido huku akiwataka wakuu wa Idara kuhakikisha wanawaheshimu wafanyabiashara kwani wao ndio wanaojenga uchumi wa Taifa.
Aidha amesema kuwa wafanyabiashara wote wanatakiwa kukaa na watu wa mapato , Halmashauri pamoja na sekta nyingine zinazohusika katika shughuli za kibiashara ili kuondoa tofauti zote zinazojitokeza na migogoro isiyo ya lazima.
Awali akijibu hoja za wafanya biashara hao ambazo zililenga kuilalamikia Halmashauri kwa kuonesha kutowajali Wafanyabiashara wake Mhe. Mwaisumbe amewatoa hofu na kuwahaidi atahakikisha anamaliza matatizo yote huku akisisitiza kuwa ndilo lilikuwa kusudi la kuwakutanisha ili kuondoa utofauti.
Vilevile ameendelea kusema kuwa ili shughuli zao ziweze kwenda kama wanavyopanga ni sharti wakanunue paspoti za kusafilia kwa wale wanaokwenda nje ya nchi mara kwa mara ambazo zinadumu kwa muda wa mwaka mzima, pia akasema kuwa paspoti hiyo inakuwa na taarifa zako zote muhimu ambazo hata ukitokewa na tatizo huko nje ya nchi utapata huduma kwa haraka zaidi kuliko wale wenye paspoti za masaa.
Kwa upande wake Ndg. Jumaa Mhina Mkurugenzi Mtendaji amewataka wafanyabiashara waendelee kulipa kodi kadri ya wanavyoelekezwa ili Serikali ipate nguvu ya kuendela kutekeleza Miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa faida ya Wanalongido na Watanzania kwa ujumla.
Hata hivyo Mkurugenzi amewataka wakuu wa Idara husika za Halmashauri kutokukaa Ofisini badala yake kutembela maeneo yote yenye changamoto ma matatizo mbalimbali na kuzitatua na ikishindikana waziwasilishe kunakohusika ili zitatuliwe mara moja.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM