Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mh. Abdala ulega amewataka wafugaji kuacha kutorosha mifugo kiholela ili kuhakikisha taifa linapata kodi yake na amewataka wafugaji waeleze nini kifanyike ili kuboresha uuzwaji wa mifugo,Mh Ulega ameyasema hayo wakati alipotembelea kiwanda cha nyama kinachojengwa Longido chenye uwezo wa kuchinja mbuzi 2000 na ngombe 50 kwa siku.
Mh. Ulega amesema mchango wa sekta ya mifugo kwa nchi yetu ni mdogo sana kulingana na rasilimali tulizonazo ,malengo yetu ni kuhakikisha mchango wa sekta hii unaonekana" alisema Mh. Ulega .
Pia mkuu wa Wilaya ya Longido Mh. Frank Mwaisumbe amesema kuwa tabia ya kukamata mifugo kiholela sio nzuri ukizingatia uongozi wa awamu ya tano chini ya uongozi Dkt Pombe Jonh Magufuli ni kuwateteta wanyonge
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM