Na Johnson Ismai
Mikataba hiyo imesainiwa na wahisani walio pata zabuni hizo mapema hii leo katika ukumbi wa J.M.Kikwete wa Halmashauri ya Wilaya Longido kwalengo la kuhakikisha kukua kwa maendeleo vijijini.
Wahisani walio saini Mikataba hiyo ni Deniko Construction Ltd ujenzi wa uzio Matale”A”58, kuunga na Engarenaibor220M kwa jumla ya Sh.53,498,126.00. SK building&Civil works LTD ujenzi wa mradi wa maji Kiserian na Orbomba kwa jumla ya Sh. 103,634,680.00. Tanchi Brothers construction co.Ltd ujenzi wa mradi wa maji Losirwa kwa jumla ya Sh.98,412,000.00 Pamoja na ukarabati wa sehemu ya kuogeshea nifugo Leran’gwa na ujenzi wa sehem ya kunywea mifugo maji Olmolog na Irkaswa kwa jumla ya Sh.37,185,163. J.J Gwakisa Limited ujenzi wa miradi ya Maji Eorendekena Namanga kwa jumla ya Sh.80,236,460.00.
Akizungumza kwenye kikao hicho marabaada ya kusaini mikataba hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Sabore Mollaimet amesema kwa kua mikataba imechelewa na mda wakuanza kazi usha tolewa utekelezaji wa miradi unaanza mara kikao kuisha wanao hitaji kwenda kuonyeshwa sehemu za kazi wataenda na pia kwakua nia ni kufanya kazi basi tufanye kazi vizuri kwa mda na kwaubora sawa na dhamani ya fedha wanazo pewa.
Mh.Sabore amemalizia kwa kuwataka kila mmoja asimame kwa nafasi yake kutekeleza majukumu yake,lazima Mkandarasi alipwe fedha yake kwa uhalali na lazima mkandarasi akabidhi kazi yake yenye viwango vinavyo takiwa kwa maana wakaguzi wata pita kukagua na kutoa taarifa pia ame washukuru wotewalio kamilisha Mchakato huu wa maendeleo ya Longido.
Hatahivyo Kaimu Mkurugenzi Bwana Dominiki Ruhamvya amewataka wakandarasi kwenda kwa mda waliopewa na kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu ili kujenga jina kwa kampuni yao pia amewaambia fedha ipo barua ziandikwe ili kuhakikisha kila mtu ana chukua fedha yake ya awali.
Aidha Mratibu wa Miradi ya wilaya Ally Msangi amesema hakuna haja ya kupoteza mda tena baada ya kusaini watu watakuwa kazini tayari kwa kwenda kuona maeneo ya kazi pia amesitiza ubora wa kazi na mda wa kukabidhi kazi.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM