Na Johnson Ismail
Approved By Joseph Peter Mkumbwa . ICTO
Katika kuhakikisha maendeleo ya naongezeka kwa kasi wilayani longido juhudi zimeendelea
kufanyika ili kuhakikisha lengo/dhumuni la mafanikio linafanikiwa kama linavyo piganiwa.
Kikao cha kusaini mikataba ya Halmashauri kwa wazabuni mbalimbali walio pita vigezo stahiki kilifanyika mapema leo hii katika ukumbi wa Halmashauri wa J.M.Kikwete (w)Longido.
Akizungumza kwenye mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji,Wakili Jumaa Mhina amesema Halmashauri iko chini kimapato hivyo nilazima kuhakikisha mapato yanapatikana kwa wingi ili Halmashauri iweze kutekeleza miradi yake.
Hata hivyo Wakili Jumaa Mhina ameendelea kusema wapo wakataji wa risiti wakiona wamesha fikisha kiwango kilicho wekwa na Halmashauri wanasitisha kutoa stakabadhi na fedha zinakuwa za kwao hali mkataba unaonyesha malipo ni asilimia 20% kwa makusanyo ya mwezi mzima, “tukiwabaini tuta washughulikia ipasavyo” pia amewapongeza wote wanao fanya kazi kwa bidii.
Zoezi la kusaini Mikataba hiyo liliendelea vizuri,Wahisani walio saini Mikataba hiyo leo ni Oakland Investment,Ndauka Investment pamoja na Kionge&Alawi Enterprises. Wahisani wengine wane(4) waliomba kusaini kwamda mwingine ndani ya siku hizi 45 kwa kushindwa kufika kwenye kikao hicho kutokana na sababu zilizoko nje ya uwezo wao.
Mkurugenzi Mtendaji Wakili Jumaa Mhina pamoja na Mwanasheria wa Halmashauri Bwana. Dominiki Ruhamvya Walimaliza kwa kusaini mikataba hiyo na kuwa taka kuwa waaminifu katika kazi ili kujenga Taifa letu “natumaini mtafanya kazi nzuri”alimalizia wakili Mhina.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM